LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Feb 18, 2019

MAREKANI YAPINGA KUSHIRIKISHWA RUSSIA KATIKA UTATUZI WA MASUALA MBALIMBALI YA KIMATAIFA

Katika fremu ya nara yake ya "Marekani Kwanza" inayotoa kipaumbele kwa maslahi ya Marekani na kupuuza maslahi ya nchi nyingine duniani, Rais Donald Trump wa Marekani anaamini kuwa siasa za kuchukua maamuzi za upande mmoja na za kibinafsi za Washington zitazidisha nguvu za nchi hiyo dhidi ya wapinzani wake.
Misimamo  na hatua hizo za Trump  zimekosolewa pakubwa na wapinzani na hata washirika wa Marekani. Kwa mfano tu Ujerumani ambayo ni nchi muhimu sana ndani ya Umoja wa Ulaya na inayoongoza kiuchumi barani humo inaona kuwa, serikali ya Trump imeharibu nyenzo na taratibu zote za mfumo wa kambi kadhaa na kuweka mbele misimamo ya kutumia mabavu katika masuala ya kimataifa.  
Wakati huo huo Washington katika kipindi hiki cha utawala wa Trump, imepuuza nafasi ya madola makubwa kimataifa kama Russia na China na kimsingi inazitambua nchi hizo kama madola ya daraja la pili. Hatua hizo za Marekani haziungwi mkono na washirika wake wakubwa wa Ulaya. 
Kuhusiana na suala hilo, katika mazungumzo yake na Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence, Kansela wa Ujerumani ameitaja hatua ya kuifutilia mbali na kuipuuza Russia katika uhusiano wa kimataifa kuwa ni kosa kwa mtazamo wa kisiasa. Pence amejibu matamshi hayo ya Markel kwa kudai kuwa, Washington inaitambua Russia kuwa ilihusika katika kukaliwa kwa mabavu Ukraine mwaka 2014 na inafanya juhudi za kuvuruga amani nchini humo kupitia hujuma za kimtandao na oparesheni za siri. Bi Merkel amepinga matamshi hayo ya Mike Pence na kusisitiza kuwa: Kwa mtazamo wa kijiografia, maslahi ya Ulaya hayaruhusu kukatwa uhusiano wote na Russia. 
Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani 
Kwa sasa kunashuhudiwa mikwaruzano na migongano katika mitizamo na misimamo ya Ulaya na Marekani katika nyanja mbalimbali. Japokuwa baada ya kuanza mgogoro wa Ukraine mwaka 2014 Ulaya ilijiunga na Marekani kuiwekea vikwazo Russia kwa lengo la kuilaizimisha ibadili misimamo yake na kukubali matakwa ya Magharibi, lakini inatambua vyema mchango mkubwa na umuhimu wa Russia katika kuyapatia ufumbuzi masuala mbalimbali ya kikanda na kimataifa  na kimataifa.  
Nchi kubwa za Ulaya hazitaki kukatwa kikamilifu uhusiano wao wa kibiashara, kiuchumi na kinishati na Moscow ilhli Washington inatilia mkazo ulazima wa kupunguzwa na hata kukatwa uhusiano huo hususan katika sekta ya gesi.  
Waitifaki wa Marekani katika Umoja wa Ulaya yaani Uingereza na akthari ya nchi za mashariki na katikati mwa Ulaya wanahitilafiana kuhusu mtazamo wa Washington kwamba kuna ulazima wa kuizidishia Russia vikwazo. Wakati huo huo madola makubwa ya Ulaya kama Ujerumani yana mtazamo tofauti na yasisitiza ulazima wa kuendelezwa uhusiano huo hususan katika sekta ya uuzaji wa gesi ya Russia barani Ulaya kutokana na umuhimu wa Moscow.  
Alaa kulli hal, katika mahojiano aliyofanyiwa katikati ya mwezi uliopita wa Januari na jarida la kila wiki la Der Spiegel, Heiko Maas Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani alisisitizia udharura wa kukabiliana na yoyote ambaye ametangaza vita dhidi ya mfumo wa kimataifa wa kambi kadhaa na kueleza kuwa: Tunahitaji ushirikiano wa aina mpya na Marekani, na kambi ya Ulaya inapaswa kuimarishwa zaidi mkabala na nchi hiyo. 
Heiko Maas, Waziri wa Mambop ya Nje wa Ujerumani 
Inaonekana kuwa, msimamo huu wa Ujerumani iwe ni kuhusiana na ulazima wa kushirikishwa Russia katika siasa za kimataifa au kuhusu suala la kupinga siasa za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja za Donald Trump, una maana ya mwisho wa umoja wa kistratijia baina ya Ulaya na Marekani na kuanza awamu mpya katika uhusiano wa pande mbili za Bahari ya Atlantic. Sifa kuu ya awamu na kipindi hiki ni mitazamo inayokinzana kuhusiana na mauala mengi ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages