Shirika la Reuters limeripoti habari ya uwepo wa ukwamishaji mambo wa Marekani kwa ajili ya kufanyika safari za kimataifa za ndege katika anga ya Korea Kaskazini.
Kwa mujibu wa shirika hilo, Marekani bado inafanya njama za kuuzuia Umoja wa Mataifa kuruhusu kufanyika safari za kigeni katika anga ya Korea Kaskazini sambamba na kufunguliwa sehemu ya safari za kimataifa za nchi hiyo ya Asia. Shirika la Reuters limebainisha kwamba hatua hiyo ya Washington ni katika juhudi za Marekani za kuendeleza mashinikizo ya vikwazo dhidi ya serikali ya Pyongyang sambamba na kukaribia mkutano wa pili kati ya Rais Donald Trump na Kim Jong-un wa Korea Kaskazini mwishoni mwa mwezi huu nchini Vietnam.
Katika miezi ya hivi karibuni, Shirika la Kimataifa la Safari za Ndege ICAO lilikuwa likifuatilia kufunguliwa njia ya anga ya kimataifa kwa ajili ya Korea Kaskazini na Korea Kusini. Kwa sasa ndege za kigeni zinalazimika kutumia njia isiyo ya moja kwa moja kutokana na kutotumia anga ya Korea Kaskazini. Duru ya kwanza ya kikao cha Trump na Kim Jong-un ilifanyika tarehe 12 Juni mwaka jana nchini Singapore ambapo pande mbili zilitiliana saini makubaliano muhimu ambayo hata hivyo licha ya serikali ya Pyongyang kuyatekeleza, Washington imekwepa kuyatekeleza hadi leo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇