NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
KIWANDA kipya cha bidhaa za ngozi cha Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL), kimetiliana saini mkataba wa ujenzi wa kiwanda hicho na kampuni za ITALPROGETTI naToscana Machine Calzature (TMC) za nchini Italia kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo Februari 8, 2019.
Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Mhandisi Masud M. Omari, alianza kutiliana saini na Mkurugenzi wa Idara ya Mauzo ya ITALPROGETTI, Bw. Sergio Dani, kabla ya kumalizia na Meneje Mwenza wa Mauzo wa kampuni ya TMC, Bw. Dniel Ferradini.
Tukio hilo lilishuhudiwa na Mkuu wa Jeshi la Magere, Kamishna Jenerali, (CGP),Phaustine M. Kasike, Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Eliudi Sanga, Mshauri Mwelekezi wa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Profesa Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo, Kuu wa Magereza Mstaafu, (CGP), Dkt. Juma Ali Malewa, viongozi waandamizi wa Jeshi la Magereza, na maafisa wa juu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii, (NSSF). Jeshi la Magereza na PSSSF ni wabia wa kiwanda hicho.
Akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mradi huo wa ujenzi, Mkurugenzi Mtendaji wa KLICL, Mhandisi Masud M. Omari, alisema kampuni hiyo ilianzishwa kwa ubia kati ya uliokuwa Mfuko wa Pesnheni PPF ambao kwa sasa majukumu yake yamechukuliwa na Mfuko wa Pensheni PSSF na Jeshi la Magereza kupitia kampuni yake yaPrison Corporation Sole (PCS).
Akifafanua zaidi alisema KLICL ilianza kutekeleza majukumu yake Mei 30, 2017 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa viwanda vya bidhaa za ngozi katika eneo la Gereza la Karanga mjini Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.
“Hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya serikali ya awamu ya Tano kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa viwanda katika awamu ya pili ya Mpango wa Maendeleo (Second Five Year Development Plan-FYDP II).” Alisisitiza Mhandisi Omari.
Alisema utekelezaji wa mradi umegawanyika katika awamu mbili ikiwa ni pamoja na uboreshaji wa kiwanda cha viatu cha zamani kilichokuwa chini ya Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la PCS.
“Uboreshaji huu ulihusu ukarabati wa kiwanda kwa kuongeza mitambo mipya ili kiweze kuongeza uzalishaji kutoka jozi 150 hadi jozi 400 za viatu kwa siku.” Alisema.
Akieleza zaidi, Mhandisi Omari alisema, uboreshaji huo ulihusisha majengo ya kiwanda, ukarabati wa baadhi ya mitambo, mfumo wa umeme na ununuzi wa mitambo mipya ambapo hatua zote hizo zimekamilika mwezi Septemba, 2018.
Awamu ya pili ya utekelzaji wa mradi, ambapo kazi ya kusaini mkataba huo imefanyika leo Februari 8, 2019 ni ujenzi wa viwanda vipya (Industrial Park), vitakavyojengwa katika eneo la heka 25 sawa na mita za mraba Milioni 1 katika eneo la Gereza la Karanga Manispaa ya Moshi
“Awamu hii itahusisha ujenzi wa kiwanda cha viatu (footwear factory) chenye uwezo wa kuzalisha jozi 4,000 za viatu kwa siku.” Alisema
Aidha alibainisha pia kutajengwa kiwanda cha kuzalisha soli za aina mbalimbali za viatu (Sole Manufacturing), zipatazo 800,000 mpaka milioni 1.2 kwa mwaka.
Sambamba na uzalishaji huo pia kutakuwa na kiwanda cha kuzalisha bidhaa mbalimbali za ngozi (leather articles) kama vile mikanda, mabegi, pochi, majacket, gloves, mipira (ya football, basketball, netball), mifuniko ya makochi na viti vya magari, (sofa and car seat covers), na kibebea silaha (pistal case).
Pia tutakuwa na kiwanda cha kuchakata ngozi (Tannery), chenye uwezo wa kuchakata futi za mraba (Sq.ft.) 13,000,000 kwa mwaka, ambazo asilimia 60% zitatumika kiwandani na 40% kwa ajili ya soko la nje.
“Uwekaji saini wa mkataba uliofanyika leo baina yetu na wakandarasi wa mitambo, kampuni za T.M.C na ItalProgetti kutoka Italia ni kiashiria kwamba sasa kazi ya utekelezaji wa mradi imeanza.” Alisema
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL), Mhandisi Masud M. Omari (kushoto waliokaa) na Mkurugenzi wa Idara ya Mauzo yaITALPROGETTI kutoka Italia, Bw. Sergio Dani, wakiweka saini mkataba wa ujenzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha bidhaa za Ngozi KLICL jijini Dar es Salaam leo Februari 8, 2019 huku wakishuhudiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Bw. Eliudi Sanga, (wakwanza kushoto waliosimama), Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Phaustine M. Kasike, (wapili kushoto waliosimama) na Mshauri Mwelekezi wa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Profesa Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL), Mhandisi Masud M. Omari (wapili kushoto waliokaa),na Meneje Mwenza wa Mauzo wa kampuni ya TMC, Bw. Dniel Ferradini. |
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL), Mhandisi Masud M. Omari (kushoto), akipongezana na Meneje Mwenza wa Mauzo wa kampuni ya TMC, Bw. Dniel Ferradini baada ya kusaini mkataba.
Mkurugenzi Mtendaji wa wa Karanga Leather Industries Company Limited (KLICL), Mhandisi Masud M. Omari, akitoa maelezo ya mradi huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSSSF, Bw. Eliudi Sanga.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Phaustine M. Kasike |
Mshauri Mwelekezi wa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda nchini (TIRDO), Profesa Mkumbukwa Madundo Angelo Mtambo |
Kamishna Jenerali Mstaafu wa Magereza, Dkt. Juma Ali Malewa (kushoto), akiwa na viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza. |
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Phaustine M. Kasike, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Bw. Eliudi Sanga. |
Baadhi ya walioshuhudia tukio hilo.
Meza kuu.
Maafisa wa vyeo vya juu wa Jeshi la Magereza.
Maafisa wa vyeo vya juu wa Jeshi la Magereza. |
Viongozi waandamizi wa NSSF |
Mhandisi Omari akisalimiana na viongozi wa juu wa Jeshi la Magereza, muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza (CGP), Phaustine M. Kasike, (kulia), akisalimiana na wakandarasi, Bw.Dniel Ferradini na Bw.Sergio Dani.
Wakandarasi, Bw.Sergio Dani (kushoto), Bw.Primo Vescovi (katikati) na Bw. Daniele Ferradini, wakipongezana.
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇