Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Jenista Mhagama akisalimiana na
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki
wakati alipokutana na watumishi wa Ofisi yake Januari 30, 2019 Jijini Dodoma
NA MWANDISHI WETU
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Uwekezaji Angellah Kairuki
amekutana na watumishi wa ofisi yake kwa mara ya kwanza tangu alipoteuliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Magufuli kushika wadhifa
huo mpya.
Waziri
Kairuki amekutana na watumishi hao mapema hii leo (Januari 30, 2019) katika
Ofisi hiyo Jijini Dodoma na kuzungumza nao ikiwa ni sehemu ya kufahamiana na
kujua ofisi hiyo.
Mkutano
huo uliohudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu
Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde pamoja na Makatibu
wakuu wa Ofisi hiyo Bi.Maimuna Tarishi anayeshughulikia Bunge na Waziri Mkuu
pamoja na Dorothy Mwaluko anayeshughulikia Sera, Uratibu na Uwekezaji.
Kairuki waliwataka watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa
umoja na uzalendo ili kujilete maendeleo nchini na kuahidi kushirikiano nao kwa
kipindi chote atakachokuwa katika Ofisi hiyo.
“Kipekee ninawashukuru viongozi na watumishi wote wa Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa mapokezi mazuri na hii
ni ishara ya umoja wenu na ninaahidi kushirikiana na watendaji wote katika
utekelezaji wa majukumu tuliyonayo kwa maslahii
mapana ya ofisi yetu na Taifa kwa ujumla,”alisisitiza Kairuki
Naye Waziri wa Nchi wa ofisi hiyo Mhe.Jenista Mhagama
alipongeza watumishi wa Ofisi yake kwa kuendelea kutekeleza majukumu na
kuwataka kuwa na uzalendo na weledi wa hali ya juu.
“Ninachoweza kusema tutaendelea kutoa ushirikiano katika
utekelezaji wa kazi za kila siku kwa kuzingatia kuwa hii ni familia moja yenye nia
moja ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mhe.Rais ili kujiletea maendeleo katika
nchi yetu,”alisema Mhagama.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana na Ajira) Mhe.Anthony
Mavunde wakati wa mkutano huo na watumishi wa ofisi yake Januari 30, 2019.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bi. Dorothy
Mwaluko.
Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji
Mhe.Angellah Kairuki akisalimiana na baadhi ya watumishi wa Ofisi hiyo
alipokutana nao Januari 30, 2019 katika Ofisi hiyo Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akizungumza na
watumishi wa ofisi yake walipokutana nao mapema hii leo
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia
Uwekezaji Mhe.Angellah Kairuki akizungumza na watendaji wa Ofisi yake (hawapo
pichani) walipokutana kuzungumza nao Jijini Dodoma, kulia ni Waziri wa Nchi
ofisi hiyo, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista
Mhagama na wa kwanza kushoto ni Naibu wake Mhe. Anthony Mavunde.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah
Kairuki pamoja na Mhe.Jenista Mhagama pamoja na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde wakiwa
katika ofisi hiyo walipokutana na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu hii leo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge na Waziri Mkuu)
Bi.Maimuna Tarishi akizungumza jambo wakati wa mkutano wao na Mawaziri wa Nchi
wa Ofisi hiyo walipokutana Januari 30, 2019 Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe.Angellah
Kairuki akizungumza jambo na Viongozi wa Ofisi hiyo alipokutana nao ofisini
kwake hii leo, wa kwanza kushoto ni Waziri wa Nchi ofisi hiyo anayeshughulikia
Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe.Jenista Mhagama pamoja
na Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde.
Baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu wakisubiri
kuzungumza na Waziri wa Nchi Ofisi hiyo anayeshughulikia Uwekezaji Mhe.Angellah
Kairuki alipokutana nao kujadili masula ya ofisi yao Januari 30, 2019. (PICHA
ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇