Wafanyakazi mbali mbali kutoka Shirikisho la Vyama vya wafanyakazi Tanzania (TUCTA) wakiwa katika maandamano ya amani ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo cha Pensheni katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii yaliyofanyika leo tarehe 7 Januari, 2019 Jijini Dodoma.
Watumishi wa ofisi ya Bunge wakipita mbele ya jukwaa kuu lililoongozwa na Mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa wakati wa maandamano ya amani ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa kulipatia ufumbuzi suala la kikokotoo cha Pensheni katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamii katika tukio lililofanyika leo tarehe 7 Januari, 2019 katika Viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇