LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 26, 2019

UPINZANI NIGERIA WASIMAMISHA KAMPENI BAADA YA KUTIMULIWA JAJI MKUU

Chama kikuu cha upinzani nchini Nigeria kimetangaza kufuta kampeni zake kwa muda wa masaa 72 kulalamikia hatua ya serikali ya Rais Muhammadu Buhari ya kumsimamisha kazi Jaji Mkuu wa nchi hiyo.
Wakuu wa chama hicho cha PDP wametilia shaka uamuzi huo wa Buhari wa kumsimamisha kazi Walter Onnoghen, siku chache kabla ya uchaguzi wa rais wa mwezi ujao wa Februari.
Jaji Mkuu nchini Nigeria ni Rais wa Mahakama ya Juu yenye jukumu la kusikiliza kesi ya kupinga ushindi wa matokeo ya urais.
Mkuu cha chama cha Peoples Democratic Party, Atiku Abubakar ameuataja uamuzi huo wa jana Ijumaa kama udikteta wa kupindukia. Amesema, "Huu ni muendelezo wa ubakaji wa demokrasia iliyopiganiwa kwa jitihada kubwa nchini."
Atiku Abubakar akiwa na Rais Abubakar
Ingawa kuna wagombea zaidi ya 70 ambao wamejitokeza kuwania kiti cha urais nchini Nigeria lakini ushindani mkali unatarajiwa kuwa kati ya Rais wa sasa Muhamadu Buhari na mgombea wa chama kikuu cha upinzani PDP Atiku Abubakar aliyewahi kuwa Makamu wa Rais.
Wapinzani wa Buhari wanamkosoa yeye pamoja na serikali yake wakisisitiza kwamba, hajatekeleza ahadi alizotoa wakati alipokuwa akipiga kampeni kuwania muhula wa kwanza hasa kurejesha amani na usalama na kuliangamiza kundi la kigaidi la Boko Haram ambalo limehatarisha usalama mpaka katika nchi za jirani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages