LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 24, 2019

TSHISEKEDI AAPISHWA KUWA RAIS MPYA WA CONGO DR

Kiongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Felix Tshisekedi amepishwa leo kushika hatamu za uongozi wa nchi hiyo akimrithi Rais Joseph Kabila aliyemaliza muda wake. Hatua hiyo inahesabiwa kuwa ya kwanza katika nchi hiyo ya katikati mwa Afrika ya kukabidhiana madaraka kwa njia ya Amani nay a kidemokrasia katika kipindi hote cha miaka 59 iliyopita.
Felix Tshisekedi aliyetangazwa mshindi katika uchaguzi wa rais wa tarehe 30 Disemba amekula kiapo mjini Kinshasa mbele ya maelfu ya waungaji mkono wake, maafisa wa seriakli na mabalozi wa nchi za kigeni.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya ndiye rais pekee wa nchi aliyehudhuria sherehe ya kuapishwa Tshisekedi, suala linaloakisi shaka iliyopo kuhusu usahihi wa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.
Pamoja na hayo, picha ya kiongozi mmoja kumkabidhi madaraka mwingine kwa amani katika nchi ambako kiongozi mpya alikuwa kichukua madaraka ama kwa mapinduzi ya kijeshi, mauaji au uasi ilikuwa na ujumbe wa aina yake.

Sherehe ya kuapishwa Tshisekedi, Kinshasa

Kuapishwa kwa Felix Tshisekedi kuwa Rais mpya wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kunahitimisha mgogoro wa kisiasa uliokuwepo nchini humo kwa miaka mingi hususan baada ya rais anayeondoka madarakani, Joseph Kabila kuahirisha uchaguzi wa rais mara kadhaa baada ya kumalizika muhula wake wa uongozi miaka miwili iliyopita.
Felix Tshisekedi aliibuka mshindi kwa kupatia asilimia 38.57 ya kura, akiwatangulia wagombea Martin Fayulu wa muungano wa upinzani wa Lamuka na Emmanuel Ramazani Shadary aliyewakilisha muungano wa chama tawala nchini humo. Hata hivyo, Martin Fayulu anadai kwamba, yeye ndiye alishinda katika uchaguzi huo kwa kupata asilimia 61 ya kura, madai ambayo yametupiliwa mbali na Mahakama ya Katiba iliyoidhinisha ushindi wa Tshisekedi.  
Wakati huo huo raia wa Kongo wanaoishi nchini Burundi wamefuatilia kwa karibu sherehe za kuapishwa rais huyo mpya na kufurahishwa na jinsi madaraka yalivyokabidhiwa kwa njia za usalama nchii humo. Mwandishi wetu wa Bujumbura Hamida Issa ametuandalia ripoti maalumu kuhusu suala hilo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages