LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 24, 2019

BARAZA LA MITIHANI TANZANIA LATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018/19, LEO, MWANAFUNZI BORA ATOKA ILBORU, ARUSHA

Dodoma, Tanzania
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.


Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma,  Katibu Mkuu wa Baraza hilo Dk. Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St. Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera).

Nyingi Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).


Dk. Msonde amesema, katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi. KUONA MATOKEO YOTE>> BOFYA HAPA

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages