LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 1, 2019

SIKU YA KWANZA YA MWAKA 2019 YAKARIBISHA WATOTO LAKI NNE DUNIANI

  • Siku ya kwanza ya mwaka 2019 yakaribisha watoto laki nne duniani
Taarifa iliyotolewa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa, (UNICEF) imesema kuwa watoto laki tatu na 95 elfu wanatarajiwa kuzaliwa leo katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa 2019.
Taarifa ya UNICEF imesema kuwa, robo ya watoto hao watazaliwa kusini mwa Asia na kwamba India inatarajiwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watoto watakaozaliwa leo kwa kuwa na karibu watoto sabini elfu ikifuatiwa na China watakakozaliwa watoto elfu 45, na Nigeria barani Afrika itashika nafasi ya tatu kwa kuzaliwa watoto elfu 26 katika siku hii ya kwanza ya mwaka mpya wa 2019.
Watoto laki nne wanatarajiwa kuzaliwa siku ya kwanza ya mwaka 2019.
Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa limeongeza kuwa, watoto hao hawatapata huduma zinazohitajika za afya na limetoa ushahidi kwa kuashiria takwimu za kuanzia mwaka 2017 zinazoonesha kwamba, watoto karibu milioni moja walifariki dunia siku hiyo hiyo ya kuzaliwa kwao na kwamba wengine milioni 2.5 waliaga dunia miezi sita baada ya kuzaliwa. Imesema vifo hivyo vilitokana na sababu zinazoweza kuzuilika.
Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa limetoa wito wa kuboreshwa huduma kwa akina mama na watoto wachanga katika maeneo mbalimbali ya dunia na kurahisisha upatikanaji wa maji safi, umeme na dawa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages