Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu(
wa pili kulia) akiangalia na huku akipewa maelezo na Afisa Misitu, John
Mtika kuhusu hatua za miche ya miti ya
miembe inavyokua wakati Naibu Waziri huyo alipotembelea ofisi za
Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya Miti mkoani Morogoro kwa lengo la kujua
imejipangaje kuzalisha miche za miti yenye ubora ikiwemo ya mbao pamoja na ya matunda ambayo itasambazwa nchi nzima Kulia
ni Mkurugenzi wa Kurugenzi hiyo, Edgar Masunga pamoja na watumishi wengine.
--------------------
NA LUSUNGU HELELA-MOROGORO
Naibu Waziri wa Maliasili
na Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu ameahidi kulifanyia kazi suala la
kugawa miche ya miti bure kwa
Wananchi ili wakaipande iliyooteshwa na
Kurugenzi ya Uzalishaji miche ya miti
kuwa utaratibu huo hauwezi kuleta matokeo yaliyokusudiwa na Serikali.
Imeelezwa kuwa uzoefu uliopo unaonesha kuwa vitu vingi
ambavyo Serikali imekuwa ikivigawa bure kwa Wananchi bila wananchi hao
kuchangia gharama yoyote vitu hivyo hushindwa kuthaminiwa.
Mhe. Kanyasu alitoa kauli hiyo jana mkoani
Morogoro wakati alipotembelea ofisi za
Kurugenzi hiyo kwa lengo la kujua imejipangaje kuzalisha miche za miti
yenye ubora ikiwemo ya mbao pamoja na
ya matunda ambayo itasambazwa nchi
nzima.
Alisema utaratibu huo itabidi uangaliwe upya kwa vile ni
ngumu kwa wananchi walio wengi kuitunza
kwa sababu hawasikii uchungu na walio wengi hujikuta wakiitupa au
kuiacha bila kuimwagilia hadi inakufa.
''Ukichukua miche leo halafu ukaipeleka mkoani Shinyanga
ukagawa bure yote italiwa na ng'ombe na vivyo hivyo ukaipeleka Dodoma yote itakufa kwa vile haitamwagiliwa
maji kwa sababu ni ya bure'' Amesisitiza
Alisema siku zote
kitu cha bure hakithaminiwi, hivyo lazima kila Mwananchi achangie kidogo lakini isiwe bure kabisa.
Hata hivyo, Mhe. Kanyasu alisema miche ya miti inaweza kutolewa bure kwa taasisi za umma
kama vile shule ila kwa makubaliano
maalumu lakini sio kwa wananchi.
Aidha, Aliitaka Kurugenzi hiyo ijiendeshe kibiashara badala
ya kujikita kutoa huduma kwa wananchi
Katika
hatua nyingine, Mhe Kanyasu aliiagiza Kurugenzi hiyo ifungue utalii
wa bustani wa miti na maua katika jiji la Dodoma ambao ni moja ya aina
ya utalii unaopendwa sana hasa na
Wanamazingira.
Alisema miji kama Arusha pamoja na Mwanza imeanzisha utalii
huo licha ya kuwa kumekosekana mwongozo wa kuziboresha bustani hizo lakini hata
hivyo watalii wengi wamekuwa wakimiminika katika bustani hizo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇