Unapoitazama filamu ya Neria, katikati ya filamu hii utalisikika gitaa likilalamika.
Na kwa namna nyuzi zinavyodokolewa kiustadi ni nadra kwa mtazamaji kutolitega sikio lake barabara ili lipate kuyanasa vema mawimbi ya sauti ya gitaa hili!
Taratibu, sauti ya nzito ya kiume, sauti akrama huungana na gitaa hilo kuzungumza na hisia za mtazamaji, katika namna inayoweza kumliza mtu mwenye machozi ya karibu.
Husikika barabara....🎵🎵🎵🎶🎶🎵🎵
Neriaaa Neriaaa oooh
Usaore moyo ka Neria, Mwari anewe ×2
Mwari anewe ka Neria, Mwari anewe kufirwa nemurume hanzvadzi, zvinoda moyo wekushingaaa
Usaore moyo ka Neria, Mwari anewe x2
Mwari anewe ka Neria, Mwari anewe
Yaani anamaanisha...
Usife moyo Neria, Mungu yu pamoja nawe
Mungu yu pamoja nawe Neria, Mungu yu pamoja nawe
Kufiwa/kuomboleza juu ya mume wako, kunahitaji moyo shupavu dada.
Usife moyo Neria, Mungu yu pamoja nawe
Mungu yu pamoja nawe Neria, Mungu yu pamoja nawe.
Ni Oliver Mtukudzi huyu! Mzimbabwe huyu!
Mwanamuziki nguli toka Barani Afrika.
Katika filamu hii, Oliver amezichonyota kisawasawa hisia za watazamaji kwa ile sauti kwa lile gitaa... aah! Kifo hiki!
"Binafsi nilianza kumjulia hapa, nilianza kutambua sawasawa kuwa gitaa pekee linaweza kuzikausha, kuzikunja na kuzinyoosha hisia likipapaswa kiustadi.
Nikaja kumsikia katika wimbo wa Todii. Nikazidi kumpenda katika wimbo wa Wasakara na nyinginezo nyingi mno ambazo kwa hakika hata pasipo kuelewa anachoimba (Alitumia lugha yao zaidi - Shona).
Niliburudika, nilihamasika kujua maana ya nyimbo zake.
Kipawa hiki! Kipaji hiki!
Katika moja ya mahojiano yake, Oliver alipata kusema; alitunga nyimbo si kwa lengo la kuburudisha tu, alitunga kufikisha ujumbe fulani.
Oliver Mtukudzi amelala usingizi wa mauti leo hii Januari 23, 2019, akiwa na umri wa miaka 66!
Kazi yake imeisha, alikuja, akatenda na sasa amerudi. Tumebaki na kumbukumbu tamu ya nyimbo zake na kazi zake nyingi za kijamii zinazoacha alama jalili kwetu.
Kwaheri Mtukudzi!".
©2019 Laura Pettie
Your Ad Spot
Jan 23, 2019
Home
Unlabelled
MWANAMUZIK NGULI OLIVA MUTUKUDZI AFARIKI DUNIA
MWANAMUZIK NGULI OLIVA MUTUKUDZI AFARIKI DUNIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇