LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 12, 2019

MAPOKEZI YA NDEGE YA PILI YA AIRBUS220-300

   Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius  Nyerere, kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Ally Bashiru, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel ,na Kulia ni Mkrugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL)  Mhandisi Ladislaus Matindi, Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe. 

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa mara baadya ya kuzindua ndege mpya aina ya Airbus 220-300 iliyowasiri leo 11 Januari, 2019 kulia ni , Mwenyekiti wa  Kamati ya Bunge ya Miundombinu Suleiman Kakoso na Waziri  wa Ujenzi ,Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe, kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Tulia Ackson na Balozi wa Canada nchini Tanzania Pamela O’Donnel







 Wafanyakazi wa Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) wakiwa wamesimama mbeleya  ndege mpya aina ya Airbus 220-300 mara baada ya kuipokea leo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ndege hiyo ni ya kwanza kununuliwa na serikali ya Afrika (Tanzania).



. Ndege mpya ya kisasa aina ya Airbus 220-300 iliyopewa jina la moja ya hifadhi ya  mbuga za wanyama  (Ngorongoro), ikikaribishwa kwa water salute mara baada ya kutua leo 11 Januari 2019 katika Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere  ikitokea Canada ilikotengenezwa. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages