LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 13, 2019

MAKUMI WAPOTEZA MAISHA KATIKA MRIPUKO WA LORI LA MAFUTA NIGERIIA

Makumi ya watu wanahofiwa kupoteza maisha katika mripuko wa lori la mafuta katika eneo la Odukpani, jimboni Cross River kusini mashariki mwa Nigeria.
Msemaji wa Polisi wa jimbo la Cross River, Irene Ugbo bila kutaja idadi kamili, amesema watu wengi sana wamega dunia katika ajali hiyo iliyotokea usiku wa kuamkia jana.
Akpan Imon, mmoja wa mashuhuda wa mkasa huo amesema binafsi ameweza kuhesabu miili 18 ya wahanga wa ajali hiyo, huku mkaazi mwingine wa eneo hilo kwa jina Sunday Ibor akisema waliofariki dunia katika mripuko huo ni watu zaidi ya 20.
Mashuhuda wengine wanasema zaidi ya watu 60 waliokuwa wakijaribu kuchota mafuta baada ya lori hilo kuripuka wameaga dunia katika ajali hiyo. Ajali za namna hii zimekuwa zikishuhudiwa mara kwa mara nchini Nigeria.
Mripuko wa Lori la mafuta mjini Lagos mwaka jana
Juni mwaka jana, watu tisa waliaga dunia baada ya lori la mafuta kuripuka katika barabara kuu kati ya Lagos na Ibadan, kusini magharibi mwa Nigeria. 
Aidha Juni mwaka 2015 karibu watu 70 walifariki huko mashariki mwa Nigeria mjini Onitsha baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto, miaka mitatu baada ya kushuhudiwa ajali mbaya sana ya moto wa mafuta iliyoua zaidi ya watu 100 huko Niger Delta, katika mkasa uliochangiwa na watu kuchota mafuta yaliyomwagika baada ya lori la mafuta kupata ajali

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages