Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ameahidi kuandaa ajira zaidi, kuboresha uchumi na kushughulikia suala la ubaguzi wa rangi nchini humo. Rais Ramaphosa ameyasema hayo akihutubia mkutano wa chama chake wa kufungua kampeni za uchaguzi wa bunge wa mwaka huu.
Uchaguzi huo unaotazamiwa kufanyika mwezi Mei utakuwa mtihani wa kumchunguza Rais Ramaphosa kama ameweza kuvutia uungaji mkono wa wananchi kwa chama chake cha ANC ambacho kimekuwa katika hatamu za uongozi tangu kumalizika utawala wa ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini mwaka 1994.
Cyril Ramaphosa alishika hatamu za kuiongoza Afrika Kusini mwezi Februari mwaka jana baada ya waitifaki wake ndani ya chama tawala cha ANC kushinikiza kujiuzulu Jacob Zuma Rais wa wakati huo, wakihofia kuwa sakata la ufisadi na kudorora uchumi wa nchi hiyo vingeweza kuathiri nafasi ya chama hicho katika uchaguzi huo wa mwaka huu.
Akihutubia maelfu ya wafuasi wa chama tawala cha ANC katika uwanja wa Moses Mabhida huko Durban, Rais Cyril Ramaphosa amesema kuwa ajenda ya chama hicho ni kuandaa ajira nyingi na kuhakikisha kuwa wafanyakazi wote wanaweza kuendesha maisha yao katika hali ya kawaida.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇