Ikulu, Dar es Sallaam
Makamu wa Rais
Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo
na mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Wa kwanza alikuwa
Balozi mpya wa Misri hapa nchini Gaber Mohamed Abulwafa Balozi mpya wa Misri ambaye alifika kwa
lengo la kujitambulisha na pia kuzungumzia mambo mbali mbali ya kuimarisha
uhusiano baina ya nchini mbili ambao
ulianzishwa na waliokuwa marais wa nchi hizi, Baba wa Taifa Hayati Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere na Rais Gamal Abdel Nasser Hussein wa Misri.
“Misri
itaendelea kutoa ushirikiano katika masuala ya Elimu, Afya na masuala ya
teknolojia ya ujenzi wa miundombinu yenye tija kwa mataifa haya mawili” alisema
Balozi huyo.
Balozi huyo mpya wa Misri
aliahidi kusimamia miradi yote ambayo ipo kwenye makubaliano baina ya Serikali
hizi.
Makamu wa Rais alimpongeza
na kumkaribisha Tanzania pamoja na kumhakikishia ushirikiano mzuri katika kazi
zake akiwa hapa nchini na kumueleza kuwa kwa miaka mingi uhusiano kati ya Misri
na Tanzania umezidi kuimarika.
Balozi wa Pili kukutana na kuzungumza na Makamu wa Rais
alikuwa ni Francisca Pedros, Balozi mpya wa Hispania hapa nchini ambaye
Makamu wa Rais alimpongeza kwa kuwa Balozi wa kwanza mwanamke kuteuliwa kuja
kuitumikia nchi yake hapa nchini.
Mwingine ni Balozi wa Ethiopia nchini Yonas Yosef Sanbe
ambaye alimueleza Makamu wa Rais furaha yake ya kuwa hapa na kuona namna
mahusiano ya nchi hizi mbili yameboreka ambapo alisema kuwa
“Nafarijika
kuona namna ambavyo wanawake wanapewa nafasi za juu katika uongozi katika nchi
hizi mbili”
Makamu wa Rais pamoja na mambo mengine alimpongeza Balozi
huyo wa Ethiopia kwa kuwa Balozi wa kwanza mwenye makazi yake hapa Tanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇