LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 14, 2019

LORI LAPONDA KUNDI LA WATU NA KUUA 20 NCHINI NIGERIA

  • Mji wa Ekiti wa kusini mwa Nigeria
Maafisa wa Nigeria wametangaza kuwa, lori moja limevamia kundi la watu katika soko moja lenye mrundikano mkubwa wa watu kusini mwa nchi hiyo na kuua watu wasiopungua 20.
Maafisa hao wametangaza habari hiyo leo Jumapili na kuongeza kuwa, lori moja limevamia soko lenye watu wengi katika eneo la Ekiti la kusini mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua 20.
Shirika la habari la Xinhua nalo limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa tukio hilo imetokea katika soko la Iverko na wengi wa wahanga wake ni wanunuzi na wauzaji waliokuweko nje ya soko hilo la mnada.
Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria

Polisi wa Nigeria wamesema wanaendelea na uchunguzi wa kugundua iwapo tukio hilo ni la ajali tu au ni shambulizi la kigaidi.
Jeshi la Polisi la Nigeria limeweka pia uwezekano wa tukio hilo kuwa la kigaidi kutokana na kuwa kwa miaka mingi sasa Nigeria imekumbwa na vitendo vya kigaidi vya genge la Boko Haram na licha ya Rais Muhammadu Buhari kuahidi katika kampeni zake za uchaguzi kuwa atawamaliza magaidi hao lakini si tu ameshindwa kutekeleza ahadi zake kwa wananchi, bali hata vitendo vya genge hilo la wakufurishaji vimeongezeka hivi sasa hususan katika jimbo la Borno la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages