LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Jan 4, 2019

KATIBU MKUU WA CCM DK. BASHIRU ALLY AZURU KABURI LA BABA WA TAIFA MWALIMU NYERERE

Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ally akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere alipozuru kaburi hill, Jana Januari 3, 2019.
------------
TAARIFA

Tarehe 3. 01. 2019
Katibu Mkuu wa CCM Dkt.Bashiru Ally amepokelewa Mkoa wa Mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera

Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally atafanya ziara ya siku mbili kuimarisha Chama Mkoa wa Mara ikiwa ni pamoja na kutembelea Wilaya ya Butiama alikozikwa mwasisi wetu Mwl. Julius kambarage Nyerere

Aidha, Ndg. Bashiru Ally amesema katika ziara yake hii ni kukijenga chama nakukiimarisha katika Misingi iliyowekwa na Mwasisi wetu Mwl.Nyerere

Ndg. Bashiru Ally  ameyasema hayo Mbele ya wananchi na viongozi wa Chama na serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama Mkoa Ndg. Samweli Kiboye (namba 3) wakikagua kituo cha Afya jimbo la Bunda

Katika ziara hiyo ameshiriki kikao cha Halmashauri Kuu  ya CCM Wilaya ya Butiama.

Katika kikao hicho Dkt.Bashiru Ally ametoa salamu za Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Mh. John Pombe Magufuli kwa wana Mara na kuwambian anawahakikishia kuwa miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa Hospitali ya Mkoa na Uwanja wa ndege wa kisasa Musoma itatekelezwa.

Katibu Mkuu wa CCM amehitimisha kikao hicho kwa kusisitiza Umoja kwa watumishi wa Chama na Serikali, kwani kwa kufanya hivyo tutakuwa tunaendeleza misingi iliyo asisiwa na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere.

Huu ni Mwendelezo Wa Uimarishaji wa Chama Cha Mapinduzi Kanda ya ziwa


Imetolewa na:
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages