LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 15, 2018

SYRIA KUREJESHEWA UANACHAMA WA ARAB LEAGUE

Bunge la Jumuiya ya Nchi za Kiarabu limeitaka Arab League iirejeshe Syria kuwa mwanachama wake, miaka saba baada ya kuvuliwa uanachama huo.
Habari hii ilitangazwa jana Ijumaa na shirika rasmi la habari la Misri, ingawaje halikutoa maelezo ya kina.
Mahmoud Afifi, msemaji wa Katibu Mkuu wa Arab League amekataa kulizungumzia suala hili alipotakiwa kufanya hivyo na shirika la habari la Reuters, lakini amekariri matamshi ya huko nyuma ya Aboul Gheit kuhusu kuvuliwa uanachama Syria.
Mwezi Aprili mwaka huu, Ahmed Aboul Gheit, Katibu Mkuu wa Arab League alinukuliwa na gazeti la Al Bayan la Imarati akisema kuwa, kwa mtazamo wake maamuzi ya kuiondoa Syria katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu yalikuwa makosa makubwa.
Ahmed Aboul Gheit, Katibu Mkuu wa Arab League
Jumuiya ya Nchi za Kiarabu (Arab League) kupitia mashinikizo mbalimbali ya nchi za Magharibi ilitangaza kusimamisha uanachama wa Syria katika jumuiya hiyo mwezi Novemba 2011.
Mgogoro wa Syria uliibuka kuanzia mwaka 2011 baada ya makundi ya kigaidi na ukufurishaji yanayopata uungaji mkono wa kifedha na silaha kutoka Saudia, Imarati, Marekani na waitifaki wao kutumwa ndani ya nchi hiyo ya Kiarabu kwa lengo la kuleta mabadiliko ya mlingano katika eneo kwa maslahi ya utawala wa Kizayuni. 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages