Mtangazaji wa TV ya Misri afichua: Kuanzia 2019 wenye paspoti za Israel wataweza kuingia Saudia
Mtangazaji na mwendeshaji mashuhuri wa vipindi vya televisheni nchini Misri amekosoa uhusiano wa karibu uliopo kati ya Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel na kufichua kwamba: Wasaudi wamewarahisishia Wazayuni kufanya safari katika ardhi tukufu za Makka na Madina.
Moataz Matar, mwendeshaji vipindi katika televisheni ya Ash-Sharq nchini Misri amesema: Kwa uamuzi uliochukuliwa na Saudia, kuanzia mwaka 2019, watu wenye pasi za kusafiria za Israel wataweza kuingia nchini Saudi Arabia; na hiyo ni habari ya kushtusha.
Matar amebainisha kuwa, baada ya Saudia kuondoa kizoro kwenye uso wake na kutangaza hadharani ushirika na uitifaki wa kihistoria baina yake na Wazayuni, uamuzi huo mpya iliochukua ni hatua nyingine ya kuutumikia utawala wa Israel.
Mwanahabari huyo mashuhuri wa Misri aidha amesema: Uamuzi huo wa utawala wa Saudi Arabia ni hatua inayolenga kuyafuta malengo matukufu ya Palestina, kwa sababu kuanzia sasa endapo Wapalestina wanaoishi kwenye ardhi zinazokaliwa kwa mabavu (Israel) watataka kutekeleza ibada ya Hija watalazimika kuwa na pasi za kusafiria za Israel.
Ameongezea kwa kusema: Laiti kama Aal Saud wasingelikuwepo, Wazayuni pia wasingekuwepo.
Tangu mwezi Septemba mwaka huu, Saudi Arabia ilianza kutekeleza sheria inayoeleza kwamba, Wapalestina wenye pasi za kusafiria za Jordan na Lebanon hawatakuwa na haki ya kwenda kutekeleza faradhi ya Hija huko Makka mpaka wawe na paspoti za nchi nyingine au ya utawala wa Kizayuni wa Israel.../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇