LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 13, 2018

MWENDESHA MASHTAKA MKUU RWANDA KUKATA RUFAA DHIDI YA DIANE RWIGARA

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Rwanda, Jean Bosco Mutangana ametangaza kuwa, atakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama wa tarehe 6 mwezi huu uliomuachilia huru mwanasiasa wa upinzani na mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, Diane Rwigara pamoja na mama yake.
Watuhumiwa hao walikuwa wanakabiliwa na adhabu ya kifungo cha miaka 22 jela kwa makosa ya kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi wa Rwanda pamoja na kughushi nyaraka.
"Upande wa Mashitaka haujaridhishwa na uamuzi wa mahakama wa kuwaachilia huru watuhumiwa hao, hivyo tumeamua kukata rufaa katika siku zijazo," Bw Mutangana amesema katika mkutano na waandishi habari mjini Kigali."
Aidha Mwanasheria Mkuu wa rwanda amesema kuwa, tulisoma kwa makini uamuzi wa Mahakama Kuu katika kesi ya Rwigara na tumeamua kukata rufaa. Tunaamini kwamba ushahidi ambao tuliwasilisha mbele ya Mahakama ya juu haukuzingatiwa kikamilifu.
Mapema mwezi Desemba, Diane Rwigara, mkosoaji mkubwa wa Rais Paul Kagame, aliachiliwa huru baada ya kufutiwa makosa yaliyokuwa yanamkabili yeye pamoja na mama yake Adeline Rwigara.
Jean Bosco Mutangana, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Rwanda
Mahakama Kuu ya Rwanda ilitangaza kwamba mashtaka dhidi yao hayana msingi wowote. Katika uamuzi wake, Mahakama Kuu ya Rwanda ilibaini kwamba ukosoaji wa Diane Rwigara dhidi ya serikali, hasa katika mikutano na waandishi wa habari, haukuwa wa "kuchochea vurugu na mgawanyiko miongoni mwa wananchi" kwa sababu ilikuwa haki yake katika uhuru wa kujieleza anayopewa na Katiba ya Rwanda na sheria za kimataifa.
Majaji pia walibaini kwamba, upande wa mashtaka haujaonyesha kwamba Diane Rwigara alighushi nyaraka alipowasilisha fomu zake za kugombea uchaguzi mbele ya tume ya uchaguzi mwaka 2017. Uamuzi wa kukataliwa kwa Diane Rwigara kuwania katika uchaguzi huo ulikosolewa na serikali za magharibi na mashirika ya kutetea haki za binadamu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages