Matokeo ya uchunguzi wa hivi karibuni kabisa yanaonesha kuwa, idadi ya mauaji yaliyotokana na ufyatuaji risasi nchini Marekani yameongezeka zaidi mwaka 2017 kuliko karibu miaka 40 iliyopita.
Press TV imekinukuu Kituo cha Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa nchini Marekani (CDC) kimetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, data mpya za kituo hicho zinaonesha kwamba, vifo vya watu 39 elfu na 773 vilivyotokea mwaka 2017 nchini humo vimetokana na ufyatuaji risasi.
Kwa mujibu wa kituo hicho, ingawa idadi ya watu wanaojiua kwa kutumia silaha za moto nayo imeongezeka nchini Marekani, lakini mauaji ya kupigwa risasi ndiyo yaliyoongezeka zaidi nchini humo kiasi kwamba haijawahi kushuhudiwa mfano wake katika kipindi cha karibu miaka 40 iliyopita.
Mwaka 2017 pia Marekani ilishuhudia moja ya mashambulizi makubwa sana ya mauaji ya umati kutoka kwa mzungu mmoja mwenye silaha kiasi kwamba mauaji kama hayo hayajawahi kutokea nchini Marekani katika historia nzima ya hivi karibuni ya nchi hiyo.
Tarehe Mosi Oktoba mwaka huo wa 2017, gaidi mmoja mzungu aliwamiminia risasi na kuwaua kwa umati na kwa mkupuo mmoja watu 58 waliokuwa wanashiriki kwenye tamasha la sanaa huko Las Vegas.
Chuki za kidini, kirangi na kikabila zimeongezeka sana nchini Marekani tangu alipoingia madarakani Donald Trump tarehe 20 Januari, 2017.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇