Waziri wa Mafuta wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Bijan Namdar Zangeneh amesema kuwa kiwango kilichoruhusiwa na Marekani kwa ajili ya wanunuzi wa mafuta ya Iran, hakilingani na mahitajio na hivyo inatazamiwa kwamba katika miezi ijayo watumiaji wa nishaji hiyo muhimu watakabiliwa na kipindi kigumu mno.
Bijan Namdar Zangeneh amesema kuwa licha ya awali Rais Donald Trump wa Marekani kuwazuia wanunuzi wa mafuta ya Iran wasifanye hivyo, hatimaye serikali ya Marekani imelazimika kukiri kushindwa kwake kuiondoa Iran katika soko la mauzo ya mafuta, kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta duniani. Amefafanua kuwa kutokana na uhaba mkubwa wa mafuta na kutokuwepo mlingano kati ya wauzaji na watumiaji wa nishati hiyo na kadhalika kwa lengo la kupunguza mashinikizo kwa watumiaji wakubwa, Marekani imelazimika kuziruhusu nchi kadhaa kuendelea kununua mafuta kutoka nchi hii. Wakati huo huo, Hossein Amir-Abdollahian, msaidizi maalumu wa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika masuala ya kimataifa amesema kuwa, Marekani haina uwezo wa kuendeleza vikwazo dhidi ya Iran na kwamba hatua ya Washington ya kuiwekea vikwazo nchi hii sio jambo jipya.
Amir-Abdollahian ameyasema hayo wakati akizungumza na balozi wa Brazil mjini Tehran, Rodrigo de Azeredo Santos ambapo sambamba na kusisitizia umuhimu wa mashirikiano ya kibunge na kadhalika kustawishwa mahusiano katika nyuga tofauti kati ya Iran na Brazil, amesema kuwa, bunge la nchi hii linakaribisha kupanuliwa mahusiano hayo ya kibunge baina ya nchi hizi. Ameongeza kwamba kusema kuwa, ushirikiano wa kibunge ni himaya muhimu kwa ajili ya kustawishwa uhusiano wa kirafiki kati ya Tehran na BrasĂlia na kwamba bunge la Iran linakupa umuhimu mkubwa kustawishwa mahusiano ya pande mbili hizo. Kwa upande wake Azeredo Santos, balozi wa Brazil mjini Tehran sambamba na kubainisha nyanja za ushirikiano zilizopo kati ya nchi mbili katika nyuga tofauti na pia nafasi chanya ya Iran katika kusimamia usalama na uthabiti katika eneo la Mashariki ya Kati amesisitiza kwamba nchi yake inakaribisha mwenendo wa ushirikiano kati ya nchi mbili. Aidha katika kikao hicho, balozi wa Brazil amesifia ustawishwaji wa ushirikiano wa kibunge wa Iran na nchi yake na kuzungumzia safari inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni ya kundi la kirafiki la bunge la Brazil nchini Iran.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇