LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 7, 2018

TAIFA STARS KUELEKEA AFRIKA KUSINI KUIKABILI LESOTHO

 Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars"  kimeondoka alfajiri ya jana kwenda Afrika Kusini kuweka kambi ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho katikati ya mwezi huu kwa ajili ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani, nchini Cameroon.


Kikosi hicho kimeondoka kikiwa na matumaini makubwa kwamba mazoezi watakayoyafanya yatawasaidia kuibuka na ushindi mchezo wao ujao dhidi ya Lesotho ugenini.

Taifa Stars watakuwa wageni wa Mamba wa Lesotho Novemba 18, mwaka huu, Uwanja wa Setsoto mjini Maseru, katika mchezo wa Kundi L kufuzu AFCON ya mwakani, itakayofanyika Cameroon.

Kikosi hicho kitaweka kambi ya siku 10 nchini Afrika Kusini kikijifua vikali chini ya Kocha wake Mkuu, Mnigeria Emmanuel Amunike na msaidizi wake, Hemed Morocco.

Wachezaji waliosafiri na Stars ni pamoja na makipa Aishi Manula wa Simba SC, Aaron Kalambo wa Tanzania Prisons, Beno Kakolanya wa Yanga SC na Benedictor Tinocco wa Mtibwa Sugar.

Mabeki ni Shomary Kapombe, Erasto Nyoni wa Simba SC, Ally Ă«SonsoĂ­ Abdulkarim wa Lipuli FC, Kelvin Yondan, Gardiel Michael wa Yanga SC, Aggrey Morris na Abdallah Kheri wa Azam FC.

Viungo ni Salum Abubakar Ă«Sure BoyĂ­, Mudathir Yahya wa Azam FC, Salum Kimenya wa Tanzania Prisons, Feisal Salum wa Yanga SC, Jonas Mkude na Shiza Kichuya wa Simba SC.

Washambuliaji ni Thomas Ulimwengu aliye huru baada ya kuvunja mkataba na Al Hilal ya Sudan mwishoni mwa wiki, John Bocco wa Simba SC na Yahya Zayed wa Azam FC.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages