Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wataalamu
mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli,
pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam
mara baada ya kuzungumza nao na kuwashukuru kwa huduma wanayoitoa nchini.
Wengine katika picha ni Balozi wa Israel hapa nchini Noah Gal Gendler wanane
kutoka (kushoto) waliosimama mstari wa mbele Naibu Waziri wa Wizara ya Afya
Dkt. Faustine Ndungulile watisa kutoka kulia mstari wa mbele.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam
Daktari Bingwa wa Upasuaji wa Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani Profesa Roger Hartl akizungumza katika kikao kilichowajumuisha Wataalamu mbalimbali wa Afya wakiwemo Madaktari bingwa wa Moyo kutoka nchini Israeli, pamoja na Madaktari wawili kutoka nchini Marekani, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia zawadi ya Kitabu alichopewa Dkt.
Akiva Tamir Mwakilishi wa Madaktari hao
kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart kutoka Israel kama Heshma Maalumu ambayo
Taasisi hiyo huitoa kwa watu Maalum.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa zawadi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Profesa Mohamed Janabi mara baada ya
mazungumzo ujumbe wa Madakatari kutoka Taasisi ya Save a Child’s Heart ya
Israel pamoja na Madaktari kutoka Marekani Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpa Barua ya Shukrani Balozi wa Israel
hapa nchini Noah Gal Gendler ili aiwasilishe kwa Waziri Mkuu wa Israel Benjamin
Netanyahu kwa ajili ya kushukuru kutokana na mchango wa Taasisi hio ya Save a
Child’s Heart.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa
Ubongo na Uti wa mgongo ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Upasuaji Ubongo kutoka
Hospitali ya Weil Cornell New York nchini Marekani Profesa Roger Hartl mara baada ya Mazungumzo
yao Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA
IKULU
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇