Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya MOI Prof Charles Mkonyi akizungumza katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface akitoa neno la ukaribisho katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu.
Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka chuo kikuu cha Weill Cornel cha marekani Prof Roger Hartl akiwasilisha mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo ,Mgongo na Mishipa ya fahamu
Madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na mishipa ya fahamu kutoka katika mataifa mbalimbali wakifuatilia mada katika kongamano la kimataifa la madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo na Mishipa ya fahamu.
Mkurugenzi wa Ubora na Uhakiki kutoka Wizara ya Afya Dkt Mohamed Mohamed wapili kutoka kushoto aikwa katika picha ya pamoja na washiriki wa kongamano kutoka mataifa mbalimbali. Wakwanza kushoto ni Profesa Charles Mkonyi mwenyekiti wa bodi ya wadhamini MOI, watatu kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface na wakwanza kulia ni Kiongozi wa jopo la wakufunzi kutoka marekani Profesa Roger Hartl. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
NA KHAMISI MUSSA
Mkurugenzi wa ubora na uhakiki wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii,
Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mohamed Mohamed leo tarehe 5/11/2018 amefungua kongamano
la tano kimataifa la mafunzo ya madaktari bingwa wa upasuaji wa Ubongo, Mgongo
na Mishipa ya fahamu katika ukumbi mpya wa Mikutano MOI ambapo mafunzo
yanafanyika kwa siku tano, siku mbili za nadharia na siku tatu za mafunzo ya
vitendo ambayo itahusisha upasuaji.
Dkt Mohamed amesema kongamano hili la tano limehudhuriwa na zaidi ya
madaktari 100 kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Ethiopia, Malawi, Namibia na nchi
nyingine za Afrika, ulaya, na marekani ambapo mafunzo yatatolewa na Madaktari
bingwa 8 wazalendo kutoka MOI na wengine 15 kutoka Marekani na Ulaya.
Mkurugenzi Mtendaji wa MOI Dkt Respicious Boniface amesema mafunzo haya yameratibiwa
na Taasisi ya MOI kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha Weil Cornel cha New York
Marekani ambapo hii ni mara ya tano kufanyika hapa Tanzania (MOI).
“Mafunzo ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee zaidi kwani wataalamu wetu
watajifunza jinsi ya kufanya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu
kwenye ubongo (Celebral aneurysm) kwa mara ya kwanza hapa nchini ,kabla ya hapo
wagonjwa walilazimika kwenda nje ya nchi kwa gharama kubwa ” Alisema Dkt
Boniface.
Dkt Boniface amesema gharama za
upasuaji huu nje ya nchi ni zaidi ya Tsh milioni 60 na hapa nchini haitazidi Tsh milioni 10 hivyo kuanza
kwa huduma hii kutaokoa fedha nyingi za Serikali na tayari Serikali imeshanunua
darubini maalum ya kufanyia upasuaji huu mkubwa.
Aidha, Dkt. Roger Hartl Mkurugenzi wa Kitivo cha upasuaji wa Ubongo,
Mgongo na Mishipa ya fahamu kutoka chuo kikuu cha Weill Cornell amesema ni
heshma kubwa kufika Tanzania kwa mara nyingine, pia kupata fursa ya
kubadilishana uzoefu na madaktari wa Tanzania na nchi nyingine duniani.
“Pamoja na mafunzo ya nadharia tutafanya upasuaji kwa pamoja kwa njia za
kisasa, hili ndilo lengo letu hasa la kuja hapa, tunataka wenzetu wa MOI na
madaktari walio mafunzoni waweze kutoa huduma hizo kwa weledi mkubwa, tumekuwa
tukifanya hivi kwa muda sasa na tunaona wanakwenda vizuri hii inatia faraja
sana” alisema Dkt Hartl.
Pia, Dkt. Hartl amesema mafunzo ya mwaka huu yanalenga kuwajengea uwezo
washiriki ili waweze kutumia teknoljia ya kisasa ya matibabu ya Ubongo na
mgongo na kuwapa mbinu mpya za upasuaji hususani kwa mgonjwa aliyeumia kwenye
eneo la mfumo wa fahamu hususani kwenye ubongo , uti wa Mgongo na mishipa ya
fahamu iliyoharibika.
Taasisi ya MOI imeendelelea kufanya mageuzi makubwa katika huduma zake kwa
lengo la kuhakikisha huduma zote za kibingwa zinapatikana hapa nchini na
kuendelea kuokoa maisha ya watanzania na nchi nyingine za Afrika ambazo
zinazoleta wagonjwa kutibibiwa MOI.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇