LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 15, 2018

MKUU WA WILAYA AWAASA WALIMU, WASIMAMIZI NA WANAFUNZI KUTOFANYA UDANGANYIFU KATIKA MITIHANI

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Kissa Kasongwa (pichani) amefanya  ziara ya kukagua maendeleo na mazingira  ya ufanywaji wa mitihani ya Taifa ya  kidato cha Nne  na cha Pili katika Shule za  Sekondari  Wilayani hapa.

Katika ziara hiyo Mkuu huyo wa Wilaya  amefanikiwa kutembelea shule mbalimbali ambapo amekutana  na kuongea na Wasimamizi, Walimu  pamoja na Wanafunzi wanaofanya mitihani na kuwaasa kutofanya udanganyifu wowote katika mitihani hiyo ili kuepuka kufutiwa matokeo na kuwajibishwa kwa walimu na wasimamizi watakaofanya hivyo.

"Nimekuja kukagua maendeleo na mazingira  ya ufanywaji wa mitihani hii ya Taifa pamoja kuwatia moyo watahiniwa wote naamini watafanya vizuri.Hata hivyo  napenda kuwausia jambo moja fanyeni mitihani hii  kwa uaminifu mkubwa ili kuepuka kufutiwa matokeo yenu.Walimu na Wasimamizi fanyeni kazi yenu kwa uadilifu, msiwape wanafunzi majibu kwani kufanya hivyo ni makosa  na mtaadhibiwa kwa mujibu wa Sheria."
Amesema Kissa.

Zaidi  ya wanafunzi 2000 wa Kidato cha Nne na cha  Pili wanafanya mitihani ya Taifa Wilayani Korogwe.

Huu ni muendelezo wa ziara ya Sekta kwa Sekta  inayofanywa na Mkuu wa Wilaya Kissa Kasongwa,katika kuhuisha dhana ya Korogwe Mpya yenye shabaha ya kuleta mageuzi bora zaidi Wilayani hapa.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages