LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 9, 2018

MADIWANI URAMBO WAWAOMBA WAZAZI KUCHANGIA CHAKULA CHA WATOTO SHULENI

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Magreth Nakainga wakibadilishana mawazo wakati wa  kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo Novemba 9, 2018.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Magreth Nakainga (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Madiwani wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kilichokuwa kikipitia taarifa utekelezaji kwa kila Kata wilayani humo.

Mbunge wa Jimbo la Urambo Magreth Sitta  akichangia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wilayani Urambo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.

Baadhi ya Madiwani wakifuatilia taarifa ya utekelezaji wa kila Kata wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Urambo Adam Malunkwi (wa tatu kushoto akifungua kikao cha Baraza la Madiwani cha kupitia taarifa za utekelezaji wa kila Kata wilayani UramboNovemba.
NA TIGANYA VINCENT-RS TABORA
BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Urambo limekubaliana kuwaelimisha na kuwahamasisha wazazi wa wanafunzi katika Shule mbalimbali za Msingi kuchangia kwa hiari chakula kwa ajili kuwajengea mazingira rafiki ya kujifunza na kufanya vizuri katika masomo na mitihani yao.

Maazimio hayo yalitolewa jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Adam Malunkwi kwa niaba ya wenzake wakati wa kikao cha Baraza hilo lililokuwa likipitia taarifa za utekelezaji wa Kata mbalimbali za Wilaya ya Urambo.

Alisema hatua hiyo inalenga kuwafanya wanafunzi wa shule za Msingi Wilayani Urambo kuwa na usikuvu darsani kwa sababu ya kupata chakula ambacho kitawawesha kutokuwa na njaa wakati walimu wanafundisha.

Malunkwi alimwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo kuendelea kutoa vibali  kwa wazazi  ambao wako tayari kuchangia kwa hiari kwa ajili ya maendeleo ya watoto wao ili waweze kupata uji na chakula cha mchana na kuwaepusha kushinda na njaa na hivyo kuwa na uelewa hafifu.

Alisema wao wakiwa ni Wawakilishi wa Wananchi kwa ngazi ya Kata watajitahidi kutumia mikutano yao kuwaelimisha na kuwahamasisha wazazi kuelewa kuwa chakula kwa watoto kinayo nafasi kubwa ya kuwafanya wafanye vizuri katika mitihani ya kujipima na ile ya kumaliza elimu ya Msingi na hivyo kuifanya Wilaya nayo kuongoza.

Malunkwi alisema katika maeneo ambayo wazazi kwa kauli moja wamekubaliana kutoa chakula kwa ajili ya watoto wao kupata uji na chakula cha mchana kumekuwepo na mafanikio , matokeo mazuri na maendeleo mazuri ya taaluma kwao.

“Sisi ni wakulima wazuri wa mahindi, mpunga, viazi, mihogo na maharage…hakuna sababu ya kushindwa kuwasidia watoto wetu wapate chakula mashuleni na kuwafanya washinde na njaa na kupunguza usikivu wakati mwalimu anafundisha darasani…kuanzia sasa Madiwani tumeamua kutoa elimu kwa watu wetu ili waweze kuchangia chakula mashuleni kwa ajili ya maendeleo ya elimu ya watoto wetu na wilaya yetu”alisisitiza.

Naye Mbunge wa Jimbo la Urambo Magareth Sitta alisema ni shule za Msingi 16 kati ya shule za Msingi 77 ndio zinatoa chakula kwa ajili ya wanafunzi na kuwaomba katika shule zilizobaki 61 kuangalia uwezekano wa kuwasaidia watoto wao ili waweze kufanya vizuri katika masomo yao.Alisema kuwa kinachotakiwa ni kuwaelimisha ili waweze kuchangia kwa hiari kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa na Serikali.

Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa aliiagiza Idara ya Elimu kuhakikisha inaongeza juhudi ili kuziwezesha shule za Msingi na sekondari ziweze kufanya vizuri na hatimaye ziwe za kwanza kimkoa na kumi bora kitaifa.

Aliwataka wadau wote wakiwemo Madiwani kushirikiana na Idara ya Elimu katika kuweka mazingira ambayo yatawezesha kuwatayarisha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages