Wagombea urais Madagascar wamemaliza kampeni zao leo huku upigaji kura ukitazamiwa kufanyika Jumatano tarehe saba.
Uchaguzi wa mara hii utashuhudia marais watatu wa zamani wakiwania wakiwani fursa ya kuiongoza tena nchi hiyo.
Uchaguzi Madagascar unafanyika huku nchi hiyo ikiwa na kumbukumbu mbaya ya migogoro ya kisiasa. Mgogoro wa karibuni kabisa ni ule wa mwanzoni mwa mwaka huu baada ya rais Hery Rajaonarimampianina kutaka kubadili sheria za uchaguzi.
Rajaomarimampianina atachuana na rais wa zamani Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina ambao kwa nyakati tofauti waliongoza taifa hilo kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi na maandamano.
Wikendi hii, vigogo hao watatu wa siasa za Madagascar, ambao ni marais wa zamani wa nchi hiyo waliendesha kampeni zao ambazo zimemalizika rasmi leo Jumatatu, Novemba 5.
Kati ya wagombea 35 ambao bado wamejizatiti katika uchaguzi huo, walifanya
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇