Na Ahmed Mahmoud, Arusha
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kufunga maadhimisho ya tamasha la mwezi wa Urithi wa Utamaduni mkoani hapa
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini hapa jana na kaimu mkuu wa mkoa wa Arusha Theresia Mahongo ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Karatu, alisema maadhimisho hayo yatafanyika wilayani Karatu kuanzia Oktoba nane mwaka huu.
Alisema maadhimisho hayo ambayo yalizinduliwa Jijini Dodoma Septemba 15 mwaka huu na makamu wa rais Samia Suluhu Hassan yaliendelea kufanyika maeneo mbalimbali nchini ikwemo Zanzibar,Mwanza na Dar es Salaam.
Alisema kabla ya kilele hicho maadhimsho hayo yatafanyika kwa siku tano kuanzia Oktaba nane hadi 12 wilayani Karatu kwenye viwanja vya mazingira ambapo yatakwenda sambamba na maonyesho mbalimbali ya kiutamaduni.
“Maadhimisho haya yenye jina la “Urithi Festival Celebrate our Heritage kimkoa yataanza kuadhimishwa wilayani Karatu kuanzia Oktoba 8 na kilele caheke kitakuwa Oktoba 13 mwaka huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid uliopo Jijini Arusha”.
Aliongeza”Maonyesho hayo yatashirikisha ngoma za makabila 10 ya mkoa huu,maigizo,kutembelea vituo mbalimbali vya utalii pamona na michezo mbalimbali ya asili”
Licha ya maonyesho hayo pia wananchi wa mkoa wa Arusha watapata fursa ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii kitamaduni ikwemo makumbusho mbalimbali na bonde la Ngorongoro kwa gharama ndogo
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇