Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Selemani Jafo akizungumza katika Mkutano Mkuu wa chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA)
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mwanahamisi Munkunda akizungumza jambo kwaniamba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma..... wakati wa Mkutano wa chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA) kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo, alisema
awali ya yoye napenda nimshukuru Mungu kwa kutukutanisha sote tukiwa wazima na pia niwakaribishe kwa niamba ya Mkuu wa Mkoa ambaye amenituma niwaambiye anawapenda sana na mjisikie mpo Dodoma na anawaomba kwa mara nyingine mrudi kwetu, nikifika hapa nimkaribishe jembe kaka yangu Mh. Jafo kwani hadhara hii ni yako karibu sana uongee na wanachama wa wauguzi Taifa kwani wanahamu ya kukusikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo awataka wauguzi wapendane popote hasa mahala pakazi nakuwaonya wengine kuto fanyiana majungu mahala pakazi kunawengine wanafanyiana majungu na kukitokea semina ya kutoka anapewa mtu huyohuyo anayemtaka yeye, naninawaomba fanyeni kazi kama Ibada ili kesho kwa Mungu utapata Dhawabu, hayo aliyasema wakati wa Mkutano wa 46 wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Waziri jafo alisema
kutoa huduma kwa mgonjwa kwa upendo, lugha nzuri mgonjwa anapata faraja na hapo muuguzi huyo anapata dhawabu kwa Mungu
Vyeo ni baadhi ya uchoyo wa viongozi wenu kunabinadamu anaroho mbaya kama nyoka anamgonga mtu bila kumla, Waziri Jafo aliendelea kwa kusema.
Hakika nawashukuru kwakunialika mimi kuwa mgeni rasmi katika Mkutano wenu ambapo awali mlipenda awe Mh. Rais wetu mpendwa Magufuli, lakini kutokana na majukumu aliyonayo mkapenda kunialika mimi kuwa mgeni rasmi nami nilipopata taarifa hiyo na kwakuwa wauguzi ninawapenda sana nikaona nisitume hata mwakilishi ili nije mimi mwenyewe hakika ninawashukuru sana sana.
Miaka yote nashiriki sherehe za wauguzi nikiwa jimboni kwangu kisalawe, tokea nikiwa Mbunge wa kawaida mpaka hivi sasa nipo Waziri, kwahiyo miaka yote nimekuwa nikishiriki katika siku ya wauguzi lakini mwaka huu Mungu alipenda kuwa nanyi.
Kwanza kabisa niwapongeze, niwapengeze kwa kazi kubwa mnayoifanya katika maeneo yenu ya kazi, nikifahamu kazi yenu nikazi muhimu sana kwa mustakabali wa nchi yetu.
Katika mamlaka ya Serikali za Mitaa Tanzania nzima kwa ujumla tunawatumshi wasiopungua laki tano na elfu hamsini katika watumishi hao takribani watumshi lakitatu na themanini naa, wastani wa asilimia 74.2, watumishi hao wanafanya kazi katika Serikali za Mitaa ambayo ninayoiongoza mimi.
Katika watumishi hao wote Tanzania nzima tunamakundi mawili makubwa, lakwanza nikundi la walimu na kundi la pili ni la Sekta ya afya, lakini katika sekta ya afya kundi kubwa ni la wauguzi.
Mh. Rais wa wauguzi na ndugu zangu wauguzi mimi binafsi katika viongozi wa awamu ya tano waliopata fulsa ya kuzunguka nchi hii kwa maeneo yote nchi nzima nimepata fulsa hiyo.
Lakini fulsa hii nimeipata kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo, lakini safari yangu ya kuzunguka nchi nzima ilikuwa nisambamba na kuongea na watumishi.
Katika ajenda kubwa ya kuongea na watumishi lengo langu ni kuwabadilisha wafanyakazi kuacha kufanya kazi kwa mazowea, kwaani nchi yetu tumekuwa tukifanya kazi kwa mazowea.
Nawale tuliokutana katika Halmashauri mbalimbali nilisema utendaji wetu wa kazi ulikuwa ni utendaji wa kimazowea zaidi, lakini mwenendo wa kuingia Serikali ya awamu ya tano, serikali hii imekuja kwa ajenda maalumu.
Naajenda hii imewekwa na watanzania, na watanzania hao hawajalishi itikadi zao za vyama vya siasa, ama itikadi zao za dini, ama makabila waliyotoka, ama ukanda wanaotokanao, ama uwezo wao wa Elimu.
Isipokuwa watanzania wote waliweka ajenda ya Serikali ya awamu ya tano, ajenda hiyo ni yakufanya mabadiliko, safari yetu mnakumbuka kunasehemu tulikoanzia, ambao watanzania wote walisema tunataka mabadiliko katika serikali ya awamu ya tano.
Na mimi Mhe. Rais ilivyompendeza yeye mwenyewe na mwenyezi Mungu alivyoelekeza, kuniteua kuhudumu katika Wizara kubwa sana kama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, kwanza kazi yangu kubwa ilikuwa ni kuwabadilisha kuacha kufanya kazi kwa mazowea
Jukumu langu kubwa nikubadilisha mtazamo wa watumishi katika mamlaka ya serikali za mitaa, imaniyangu ni nini? nikubadilisha mwenendo wa utendaji kazi, lakini naomba hiwathibitishie hapa wauguzi mnaonisikiliza.
Katika zunguka yangu yote na kufanya tathimini nijinsi gani, niwathibitishie kwamba wauguzi ninaokutana nanyi katika mkutano wa 46, ukifanya tathmini ya 2014-2015 na 2018 tulionao leo hii utendaji wa kazi katika sekta ya afya imebadilika kwa kiwango kikubwa sana.
Nafahamu katika sekta ya afya asilimia 60 ni wauguzi lakini huduma zote zinazofanyika asilimia 80 za kazi zinafanywa na wauguzi, kwahiyo ukizungumza utendaji wa kazi umebadilika kwa kiwango kikubwa nchini mwetu nawashukuru wauguzi hongereni sana.
Sizungumzii hapa kinafki nazungumza hapa kwa ukweli na dhati na nikijua kaziyenu ni nzito mnoo , hakuna watu wanaofanya kazikubwa sana na kazi ya kiroho kama ya wauguzi .
Wauguzi wengine sura zao zaonekana za mashaka nikutokana na stress zinatokana na kufanya kazi masaa 24, naomba niwaambiye muuguzi anapoamka asubuhi kwenda kazini, akifika kazini kaziyake anainza.
Inawezekana Dkt anapoingia kufanya kazi anamasaa yake lakini muuguzi anapompokea mgonjwa anakaa na mgonjwa dkt anapofanya kazi anamuandiki dawa mjonjwa anondoka mgonjwa anabaki na muuguzi kumuangalia mpaka saa ya mwisho, Nahata vifo vingene vinatokea ni kwa bahati mbaya.
Wakati mwingine muuguzi anatamani akaye na familia yake anashindwa, kwa maana kama kuna upako wa Mungu, wauguzi wanaupako wa Mungu, naomba niwaambie wauguzi, kama kunamshahara ni
jambo moja kubwa sana nimalipo kwa mungu na nilisema haya maneno maeneo mbalimbali.
Watuwengine wanasemehewa kwa kutoa sadaka sana na zambi zingine zitafutwa kwa ajili ya kusali au kuswali sana, lakini kunadhambi zingine Mungu anasamehe kulingana na kazi zenu mnazozifanya mnasamehewa dhambi zenu na kuuona ufalme wa Mungu.
Licha ya kazi mnayo ifanya kaziyenu ina thamani kubwa sana mbele za Mungu,na mimi nawaombea sana, Mwenyezi Mungu awalipe ziada, awafanyie kila aina ya wepesi, awape roho safi , nilifika sehemu moja nilikutana na muuguzi mmoja ile wodi kwa bahati mbaya sana inataa nyingi lakini taa inayowaka ipo mlangoni peke yake, taa zingine zote haziwaki na Hospitali ina kiongozi wake, mgonjwa amezidiwa anataka kumchoma sindano.
Inabidi muuguzi akamchukuwe mgonjwa alipo amlete kwenyetaa amchome sindano halafu amrudishe alipokuwa.
Amekuja mama mjamzito kujifungua gloves zote zimekwisha , muuguzi anamsaidia huyu mgonjwa hata gloves hajavaa bila kujua huyo mgonjwa anamatatizo gani aliyonayo, lakini muuguzi kwa moyo wa huruma alionao anaona bora amuokoe huyu mgonjwa
Nahata wauguzi wengine wanapata magonjwa sio kwa hiyari yao wenyewe mazingira wanayo fanyia kazi, waguguzi niwaambiye msg ilipoingia saa saba usiku nilisema nitakuja nitafuta mambo yote.
Wauguzi wanafanya kazi kwa umakini sana na wakati huu ninaozungumza hapa wengine roho zinawauma wamepata magonjwa yasiyokuwa na tiba wapo humu ndani
Ndiyo maana nasema kazi yenu nikazi kubwa sana,nikazi mnayokaa na wagonjwa na hatawakati mwingine unaangalia mgonjwa kwa umkini pia nimeona bora niwaombe wenzangu wengine na viongozi mbalimbali.
Tuwatibu vyema watu wa Idara ya afya, hatupaswi kufanya maamuzi ya haraka inawezekana umefika mahali umekuta jambo kumbe mtu amepata stress na amefanya jambo kwa ajili ya stress, lakini mimi nawashukuru kupitia risala yenu.
Nimeyapata yale mliyoyasema nadhani mtajadili kikao hiki ndani ya siku nne au tano, na mimi nitaomba nipate maazimio baada ya mkutano wenu, yale yatakayopaswa kwetu sisi tutaendelea kutekeleza kuyafanya kwa maslahi mapana ya wauguzi nahoja kubwa nimeona hasa changamoto ya idadi ndogo ya wauguzi.
Hili mimi naomba tulichukue kama Serikali na juzijuzi hapa tuliajiri watu wa kada mbalimbali takribani hasa kipindi hiki ya sekta ya afya watu elfu nane walipata ajira ipochini
Wauguzi wa Taasisi ya Mifupa MOI wakiwa katika picha ya pamoja waliofika katika Mkutano wa chama cha Wauguzi
Baadhi ya wajumbe
Baadhi ya wajumbe wakiwa juu na wengine wakiwa chini wakimzikiliza mgeni rasmi
Waziri Jafo (wapili kushoyo) akizingua Tovuti ya Chama hicho
Your Ad Spot
Oct 3, 2018
Home
Unlabelled
WAZIRI JAFO ATEMA CHECHE MKUTANO WA 46 WA CHAMA CHA WAUGUZI TANZANIA (TANNA)
WAZIRI JAFO ATEMA CHECHE MKUTANO WA 46 WA CHAMA CHA WAUGUZI TANZANIA (TANNA)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇