Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imesema kuwa inayo azma ya kulipatia jeshi la polisi vitendea kazi kwa lengo la kukabiliana na changamoto za uhalifuu nchini humo.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Ahmed Masauni katika kikao cha wadau wa sekta ya utalii na maafisa wa jeshi la polisi, huko Kikwajuni Unguja, visiwani Zanzibar, ambapo pamoja na mambo mengine amesisitizia kukomeshwa madawa ya kulevya katika sekta ya utalii.
Hayo ni baada ya kutolewa malalamiko juu ya kuwepo vitendo vya ulanguzi za mihadarati kati sekta hiyo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇