Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo ameagiza Mganga wa wodi ya wazazi katika Hospitali ya Wilaya hiyo Abdallah Kipeta kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi kufuatia tukio la kufariki mama mjamzito kutokana na uzembe wa kutompatia huduma za matibabu kwa wakat
Agizo hilo amelitoa jana, kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Newala, wakati akizungumza na watumishi wa Afya na Wajumbe wa Bodi ya Afya kwa lengo la kuwahimiza kufanyakazi kwa weledi na kuwahudumia wagonjwa bila ubaguzi.
"Nimesikitishwa sana na kifo cha huyu mama, alikuja hapa nesi akawa anahangaika kupiga simu lakini kila mganga anayepigiwa anasema siyo zamu take, sasa yule alitekuja alikuwa amechekewa sana had I mama yule akafa.
Sasa huyu mama aliyekua ameacha kichanga eti ndiyo mnachangachanga vihela kukinunulia maziwa, kufanya hivyo ndiyo kutarudisha uhai was huyu mama? Naagiza Mkurugenzi mwandikie barua ya kumsimamisha kazi huyu Daktari halafu nipate nakala Mara moja, kama mlizoea kubebana Mimi kwangu hapana, sins mbeleko wala shuka", alisema Mkuu Hugo was wilaya.
" Hospitali hii inachangamoto nyingi sana, haina dawa, mashuka huku waiguzi hawajali wagonjwa, imefikia hatua hata bombs ya sindano mgonjwa anaambiwa hakuna, anaambiwa akanunue kwenye duka la dawa hapo nje, na hili duka lipo bize kwelikweli, vipi mna ubia nalo?" Alisema na kuhoji.
"Inasikitisha kuona kwamba huduma zinazorota kwenye hospitality hii, mkiulizwa mnasema hakuna pesa, lakini pesa za kulipana safari na semina mnapeana, sasa mnazipata wapi", alihoji.
Alisema kitendo cha wauguzi kutowajali wagojwa na kuwatolea kauli mbovu na ukosefu wa dawa kimesababisha wagonjwa wengi kutojitokeza kwenda kupata huduma za afya na hivyo kufanya mapato ya hospitali hiyo kushuka tofauti na ilivyokuwa zamani.
"Hospitali hii sasa inaonekana mnajali pesa badala ya utu, mgonjwa akitoka nchi jirani ya Msumbiji mnamkimbilia kwa sababu mnamuna atawapa rushwa, lakini akitoka Mnyambe au Kitangale hamumjali, hii tabia lazima ikome kabisa", alisema Mkuu huyo wa Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya alihitimisha kwa kutoa mwezi mmoja kwa uongozi wa hospitali hiyo kujenga choo kilichoboka kwenye wodi ya wazaxi ambapo sasa wagonjwa kwenye wodi hiyo wanajisaidia nje.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇