Na Ofisi ya DC Arumeru
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro, amefanya ziara ya kushtukiza katika Ofisi za Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) na kuzungumza na wafanyakazi na baadhi ya wananchi aliokuwa wakisubiria huduma.
Muro amelazimika kufanya ziara hiyo kufuatia kuongezeka kwa malalamiko ya wananchi dhidi ya Shirika hilo la NSSF hatua ambayo imeonekana kuwa kero sugu katika ofisi hizo zinazosababishwa na baadhi ya watumishi wachache kutokutimiza wajibu wao ipasavyo.
Akizungumza na wananchi hao wamemlamikia kuwa Shirika hilo kwa kucheleweshewa stahiki zako za mafao kwa zaidi ya miezi tisa ungali wameshamaliza taratibu zote za malipo.
Mwananchi mmoja Suleman Mzigwa amemueleza Mkuu huyo wa wa wilaya kuwa ana zaidi ya miezi akifuatilia malipo katika ofisi hizo za NSSF huku Meneja kituo hicho cha Usa River akimtolea majibu ya kejeli kila Mara afikapo kituoni hapo kufuatilia stahiki zake.
Kutokana na changamoto hiyo DC Muro amewataka watumishi wote wa Taasisi za umma kufanya kazi kwa moyo wa kizalendo huku wakitanguliza maslahi ya Taifa mbele ambapo amesisitiza kuendelea na ziara zake za kushtukiza katika *Taasisi, Mashirika, Wakala, na Idara Zote za Serikali zinazofanya kazi Wilaya ya Arumeru.
Akihitimisha ziara yake katika Ofisi za NSSF amewataka wanachama wa Mfuko wa NSSF kuendelea kuwa na imani na Shirika lao la NSSF na kusisitiza Shirika hilo kwa sasa limepata uongozi Mpya chini ya Mkurugenzi Mkuu Wakili Msomi Ndg. William Eriyo ambaye Serikali imemuamini na kumpa dhamana ya kuliongoza Shirika hilo kwa mafanikio hivyo ni imani yetu Arumeru nayo itakwenda kutazamwa kwa jicho la karibu zaidi ambapo pia amewapongeza baadhi ya watumishi wachache wanaofanya kazi kwa moyo wa kizalendo.
Your Ad Spot
Oct 6, 2018
Home
Unlabelled
DC MURO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NSSF ARUMERU
DC MURO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA NSSF ARUMERU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇