Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Yemko Vicoba vya Kiislamu Tanzania, kuanzia kushoto ni Amiri wa Wilaya ya Kinondoni Baraza Kuu la Jumuiya na Mratibu Mkuu wa Vicoba vya Kiislamu, Aboubakri Abdul-swamad na Mkurugenzi Yemco, Mohamed Bassanga
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo,kulia ni Sheik wa Wilaya ya Ubungo, Maulidi Kidebe na kushoto ni Mkurugenzi wa Yemco, Mohamed Bassanga. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
NA KHAMISI MUSSA
Sheikh wa mkoa, Alhad Mussa Salum nitawaletea gari Kituo cha watoto yatima cha, Tulee Yatima Tanzania tuyata, kituo kimenihamasisha zaidi waliniambia wanawatoto zaidi ya 460, niwatoto wengi sana hivyo niliwaahidi palepale nikawaambia nitawatafutia gari kwa ajili ya kituo chenu.
Basi nilipofika katika kituo hicho baada ya kuwaona Tuyata nikaona ndio riziki yao ili liweze kusaidia kituo hicho, aliitoa ahadi hiyo wakati wa uzinduzi wa Yemko Vicoba vya Kiislamu Tanzania na pia alipata kutoa salamu za Mufti.
kwanza kabisa niwaalikeni kwa niaba ya kipenzi chetu, Mufti Mkuu, Sheikh Abubakary Zubeir sherehe za Maulidi mwaka huu zinatarajiwa kufanyika Kitaifa Korogwe Mkoani Tanga na zinatarajiwa kufanyika tarehe19 itakuwa Ijumaa Tatu mwezi ujao wa 11 ambapo itakuwa siku ya Ijumaa Tatu na mapumziko yatakuwa tarehe 20, kwa kawaida tukisoma Maulidi siku ile inakuwa ni mapumziko na siku inayo fuata kwani ni heshima kubwa watanzania.
Waislamu tumeipewa, Lakini kwa Mkoa wetu wa Dar es Salaam kama kawaida tarehe hiyohiyo tarehe kumi na tisa wakati kitaifa inasomwa Korogwe na Dar es Salaam usiku Kimkoa tutasoma Mnazi Mmoja kwa maana kumi na tisa kwa hiyo niwaalikeni, watanzania waislamu wa mko wa Dar es Salaa nyote niwaalikeni ikiwa Serikali imetupa heshima.
Taifa linapumzika kwa sababu ya Waislamu wanasherehekea kuzaliwa kwa Mtume wao Muhamadi (S.A.W) iweje sisi tunalala kwani hiyo niheshima kubwa kwahiyo nilazima tuonyeshe kwamba serikali imetupa heshima hiyo na sisi tuonyeshe kukienzi kituchetu, kwahiyo Tarehe kumi na tisa karibuni sana, ''aliendelea kwa kusema Alhad"
Kumiliki uchumi ndio Dini, kwamba dini kama hukumiliki uchumi inakuwa ni mtihani mkubwa hata mwenyezimungu alianza kwa kutaja mali ni uchumi, ili wewe ukaye vizuri na familia yako lazima uwe na uchumi uhakikishe watoto wanakula vizuri, Familia inakaa vizuri inavaa vizuri watatekeleza dini yao sawasawa lakini na Jamii yako kwa ujumla.
Jamii yetu ikiwa ni jamii ya kimasikini haitaweza kutaharaksi hasa katika ulimwengu wa leo, ulimwengu wa Sayansi na Teklonoji ambao umeendelea sana mwenye nguvu niyule atakaye miliki uchumi atafanya atakacho katika ulimwengu na wewe usiye kuwa nacho atakufanyasa atakavyo
Kwa hiyo ulimwengu huu unahitaji kumiliki uchumi na Mtume (S.A.W) yeye mwenyewe alipiga vita umaskini na kuna dua hasa kwa kujilinda kwa Mwenyezi Mungu na ufakiri, ufakiri unauwa, ukafiri ni nusu ya ukafiri unaweza kulazimishwa kufanya mambo na ukayafanya yakumkufuru Mwenyezi Mungu kwa sababu tu ya ufakiri wako
Mtu anaweza kuichezea Imani yako kwa sababu ya ufakiri wako, nijambo ambalo tunatakiwa kulipiga vita nilazima tujikombowe katika swala zima la ufakiri
Lakini kama tunavyojuwa kwamba sisi tupo Duniani, Mwenyezi Mungu ametuweka katika dunia hii ametupa nafasi yetu akasema wazi usisahau ile nafasi yako katika dunia, unanafasi wewe.
Unanafasi ya kuwa wewe kutulia katika maeneo matatu, kwanza uwe na makazi mazuri, una nyuma nzuri unaishi, uwe na usafiri, unatoka nyumbani unakwenda Msikitini, na uwe na mke mwema, uwe na mke mwema sio mke mzuri,uwe na mke mwema kwani kunauzuri na mwema ni vitu viwili tofauti, na kama wazuri mjini wamejaa
Ukikosa mwanamke mzuri dunia unaweza kuiona jahanam mzuri kwa maana ya mwema, na ndio maana Mtume akasema mwema kwa hiyo usitafute mzuri tafuta mwema kwa maana hiyo ni dunia.
Yemco wanachokifanya wanatutafutia ile dunia yetu, nilazima tuwe na maisha mazuri hapa duniani na akhera tuwe na maisha mazuri ile habari ya kusema dunia siyetu, duni ni jela ya kila muumini na pepo ya kafiri kwani hayo ni maneno gani Sheikh.
Kwamba dunia kwetu waislamu ni jela kakwambia nani? alihoji Alhad, sisi tumeletwa duniani tuje kumuabudu mwenyezi mungu S.W na tuishi vizuri kama atakavyo Mwenyezi Mungu, hata hiyo zuhd si kwa maana usiwe na kitu maana yake uwe na kitu na kisikufanye ukamsahau Mwenyezi Mungu sio kuwa wewe ni daruweshi wewe na tasbihi kutwa kucha hutaki kuhangaika hutaki kufanya kazi
ukasema hatutaki dunia
Hapana tupo duniani mema maisha mazuri na akhera pia maisha mazuri, ndivyo Mwenyezi Mungu anatutaka tuwe, lakini ukiangalia pia hata wao Manabii hakuna aliyekaa bure kwa kila mmoja alijishughulisha kwa ajili ya kutafuta
nzima na hata katika mana bii hakuna aliyekaa bure kwani kila mmoja alijishughulisha kwa ajili ya kutafuta, ukimuangalia Adam alikuwa ni mkulima, alifanya kazi, ukimuangali Idrisa alikuwa ni fundiwa kushona, alifanya kazi, ukimuangalia Ibrahim alikuwa ni fundi wa kujenga,ukimuangalia, Zakari alikuwa ni fundi selemara alifanya kazi na ukimuangali Mtume wetu Muhamadi alikuwa mfanya biashara
Wote hao manabii walifanya kazi za kujiletea kipato na kuchochea maendeleo, kwa hiyo Yemco Taasisi ambayo inajishughulisha na kuwawezesha sisi waislamu, tukiwa kama wajasiliamali wadogo wadogo tuweze kujikim na hasa mimi niwa shukuru sana
Yemco kwa kulenga jambo hili kuanza na Maimamu, kwa sababu maimamu ndio waalimu wa waislamu na ndio viongozi wa waislamu, maimamu wakilielewa jambo waumini bila shaka watalielewa kupitia misikiti yao, watasema hayo kwa sababu wao ni wanafunzi wazuri na watakuwa ni walimu wazuri kwa wengine
Kwa hiyo Bassanga nashukuru sana umeona jambo hili wenyewe ni maimamu na umeanzia kwa maimamu, lakini pia na kwa sababu ninakazi nyingine hapa ya harambee na harambee inahitaji muda wa kutosha nitoe salamu za Mh. Mufti, wakati nakuja huku nilimjilisha kwamba nimealikwa mahahala
kunashughuli moja mblili tatu, akaniambia kwanza akiishukuru hii Taasisi ya Yemco, lakini anawashukuru maimamu walioshiriki katika jambo hili na wadau wengine kupitia njia hii ya Vicoba.
Mh. Mufti sikuzote anauchungu sana juu yakuona kwamba waislamu wanaongokewa katika mambo yao, ile sifa ya Mtume Muhamadi (S.A.W) kwa yale mambo yanayo wasumbua waislamu yana mkosesha usingizi.
Mufti na sikuzote anapupa ya kufanikiwa mafanikio ya waislmu kwa waumini Mtume alikuwa mpole kisha mwenye huruma na ndivyo alivyo Mh, Muft.
Ni katika sifa za Mwenyezi Mungu , neno jitambue linasifa zake kadha tujitambu tubadilike tuache mazowea anawena kuzigawa katika wajawake, kwahiyo Mh. Mufti anaunga mkono juhudi hizi na kauli mbi ni Jitambue, Badilika, Acha mazowea na kila kauli katika hizo
Ninilipo tembelea Bidhaa nimehamasika kwa juhudi za akina mama wanazo zifanya natamani Bi Esha angelikuwa amefika ningetembelea pamoja na nikamwambia Bassanga nitakuletea Waziri, waziri wa Viwanda na Biashara na nitamuomba aje ajionee kazi za akina mama
Kazi wanazo zifanya ni kubwa sana ni juhudi za kuunga mkono Serikali ya awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli, anataka wafanyakazi, anataka watu wanyonge wawezeshwe wawe na viwanda vidogovidogo, wafanya Biashara, sikuzote amekuwa asisimami watu wa namna hiyo
Sasa lau Waziri wa viwanda na biashara akiwaona naamini atajuwa ni namna gani ya kuwasaidia, kwahiyo hilo tutashirikiana na kuhakikisha kwamba nasi kama waislmu ni sehemu ya jamii ambayo inaunga mkono Serikali ya Dkt. John Pombe Magufuli kuhakikisha kwamba Tanzania ya Viwanda Tanzani ya uchumi wa kati inawezekana na waislamu tuhajijishe tunasimama kupiga vita umasikini
Mipango mingine ni wakubwa kuwanyonya wadogo nilazima tuone wafanya biashara wanapunguziwa utitiri wa kodi wakati mwingine naona ni mipango ya wakubwa kuwanyonya wadogo na pia niwashukuru Amana Benk hasa kwa kuhakikisha mambo yanakuwa sawa ya jamii hasa ya kiislmu
Hayatetereki.
Wamekuwa wakiwadhamini waislamu mambo yao mbalimbali na kuona waislamu wanakuwa wengi kwa kuwanusuru na riba, hivyo niwahimize kufungua akaunt ya Amana Benk kufanya hivyoi nikuifany Taasisi hiyo ili iweze kufanya kazi vizuri
Riba nikatika madhambi ambazo Mwenyezimungu anasamehe na kamauliwahi kula riba huko nyuma usidhani Mwenyezi hatakusamehe, Mwenyezi Mungu atakusamehe
Baadhi ya Maimamu wakimsikiliza Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum
BI Esha Sururu akizungumza jambo katika uzinduzi huo
Baadhi ya akina mama wakimsikiliza Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum
Baadhi ya wadau katika uzinduzi huo wakimsikiliza Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum akiendesha harambee katika uzindizi huo
Mkurugenzi wa Yemco, Mohamed Bassanga (wa pili kushoto) akiwaonesha wadau mkoba kabla ya kuzinduliwa na Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum, (kulia) kushoto ni Amiri wa Wilaya ya Kinondoni Baraza Kuu la Jumuiya na Mratibu Mkuu wa Vicoba vya Kiislamu, Aboubakri Abdul-swamad
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum akitamka rasmi kuzindua Yemko Vicoba vya Kiislamu, kushoto ni Mkurugenzi wa Yemco, Mohamed Bassanga
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti Amiri wa Wilaya ya Kinondoni Baraza Kuu la Jumuiya na Mratibu Mkuu wa Vicoba vya Kiislamu, Aboubakri Abdul-swamad kwa kuutambua mchango wake, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Yemco, Mohamed Bassanga na kushoto kwa Alhad ni Sheik wa Wilaya ya Ubungo, Maulidi Kidebe
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum akikabidhiwa zawadi na Yemko ikikabidhiwa na Mkurugenzi wa Yemco, Mohamed Bassanga kushoto, Mratibu Mkuu wa Vicoba vya Kiislamu, Aboubakri Abdul-swamad kulia na kushoto kwa Alhad ni Sheik wa Wilaya ya Ubungo, Maulidi Kidebe
Meneja wa uwezeshaji Mikopo Midogo wa Benk ya Amana, Zaki Muhidin akizungumza jambo katika uzinduzi huo
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wajasiliamali
Mweyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam ambaye pia ni Sheikh wa mkoa huo, Alhad Mussa Salum katika picha ya pamoj na viongozi
Your Ad Spot
Oct 18, 2018
Home
Unlabelled
ALHAD MUSSA SALUM ATOA AHADI YA GARI KITUO CHA TULEE CHA WATOTO YATIMA
ALHAD MUSSA SALUM ATOA AHADI YA GARI KITUO CHA TULEE CHA WATOTO YATIMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇