Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama, (wapili kulia), Naibu Wake, Mhe. Stella Ikupa (wakwanza kulia), Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), Bw. Masha Mshomba (mwenye miwani), wakiangalia jinsi wanafunzi wasioona wanavyotumia mashine maalum za kuandika nukta nundu, kwenye chou cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam Septemba 17, 2018. Waziri Jenista amepokea mashine hizo maalum Braille Machines, 11 zilizotolewa na WCF ikiwa ni utekelezaji wa sera ya kusaidia jamii (CSR) ili zitumike kwanye taasisi za wanafunzi wasioona.
NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAZIRI
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, (pichani), ameziagiza taasisi za umma na binafsi nchini
zinapotoa fedha za kusaidia jamii (CSR), zikumbuke kuna kundi maalum la
walemavu nchini ambao nao wanahitaji huduma maalum kama wanavyohitaji wengine.
Mheshimiwa
Waziri aliyasema hayo jioni ya Septemba 17, 2018 wakati akipokea mashine maalum
za kuandika kwa wanafunzi wasioona (Braille Machines) kutoka Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi (WCF) kwenye chuo cha walemavu Yombo jijini Dar es Salaam.
“Tunapoona
kwenye shule za msingi wanahitaji madawati, tukumbuke kwamba, wapo wanafunzi
kwenye vyuo, wapo wanafunzi kwenye shule
za msingi, ambao ni wenye ulemavu ambao pengine badala ya madawati, wao
wanahitaji viti vya kuwaongezea mwendo, au kama tunatoa computer mpakato,
tukumbuke kwamba tunazo shule na vyuo watoto wetu, vijana wetu wanasoma wenye
ulemavu wangehitaji mashine hizi zenye kuandika nukta nundu ili kuwasaidia
wenye ulemavu ili na wao wafaidike na elimu katika nchi yetu ya Tanzania.”
Alisema Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama wakati akihutyubia kwenye hafla ya
kukabidhi mashine hizo.
Alisema,
Amefarijika kuona maagizo ya Ofsii ya Waziri Mkuu, yameweza kutekelezwa na
taasisi ambayo iko chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, kwa kusaidia kundi hilo la
wenye ulemavu.
“Vifaa
nitakavyovikabidhi leo ni maalum kwa wenzetu wasioona na ni vya wanafunzi walioko katika vyuo
mbalimbali kwenye nchi yetu siyo hapa Yombo peke yake.” Alifafanua.
Aliupongeza
Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa msaada huo mkubwa na kwamba fedha
walizotumia kununua vifaa hivyo ni kuwekeza kwa vijana ili kujiandaa kuwa na
utashi na weledi na kujiandaa kuingia kwenye soko la ajira nchini.
Akimkaribisha
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Mhe. Stella Ikupa, ameitaka jamii ya watu
wenye ulemavu nchini kujiamini, kujitambua, kujikubali na kutioa bidii katika
kazi wanazofanya.
“Kama
ni mwanafunzi weka bidii katika masomo, na kama ni mwajiriwa weka bidii katika
kazi yako kwani huo ndio ukombozi kwa mtu mwenye ulemavu.” Aliasa Mhe. Ikupa.
Alisema
vifaa vilivyopokelewa ni muhimu sana kwa watu wenye ulemavu hususan kwa kundi
la wasioona, kwani vitawawezesha katika dhama nzima ya ujumuishwaji mtu mwenye ulemavu
anapopatiwa vifaa vinavyoweza kutekeleza majukumu yake anakuwa anawezeshwa kuwa
katika ujumuishwaji kwa hiyo atajumuishwa katika elimu lakini hatimaye
atajikuta amefikia kwenye eneo la ajira na hatimaye kujikomboa na kuon dokana
na utegemezi na uombaomba.
“Nikiwa
kama Naibu Waziri ninayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu, nitoe
pongezi za kipekee kwa uongozi wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi kwa tendo hili
kubwa ambalo mmelifanya.” Alipongeza.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF) Bw. Masha
Mshomba alisema, Mwaka jana (2017) WCF ilifanya Mkutano wa kwanza wa mwaka na
katika mkutano ule Mfuko uliahidi kupitia mpango wake wa kusaidia jamii (CSR)
utasaidia watu wenye ulemavu na kwamba ahadi hiyo imetekelezwa.
“Tumetoa
msada wa mashine hizi maalum (Braille Machines) 13 zenye thamani ya Shilinhgi
Milioni 33.8 na tunaimani kwamba zitawasaidia sana wenzetu wasioona ili
kuwafanya washiriki kwa ufanisi katika kujifunza.” Alisema.
Alisema,
Sekta ya Hifadhi ya Jamii, WCF ikiwa ni miongoni mwa sekta hiyo, moja ya
majukumu ambayo serikali inasisitiza ni kuhakikisha ushiriki wa sekta katika kuondoa
changamoto kwenye makundi maalum na hatua hiyo ya kutoa msada ni utekelezaji wa
maagizo hayo ya serikali.
Katika
awamu hii ya kwanza taasisi zilizofaidika ni pamoja na Chuo cha Ufundi kwa Walemavu, Yombo na Sabasaba kilichoko Singida, Shule za Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Shule ya Msingi Ndanda, iliyoko Mkoani Mtwara, Shule ya msingi Biharamulo, Shule ya Msingi Mgeta Mseto Bukoba Mkoani Kagera.
Mhe. Waziri Jenista Mhagama (kushoto), akiwa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia masuala ya wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, wakati akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mhe. Stella Ikupa, (Kulia), akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kwenye chou cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, wakiwa kwenye hafla ya kupokea msada wa mshine za kuandika nukta nundu (Braille Machines)
Wanafunzi wakijadiliana wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine za kuandika nuka nundu (Braille Machines) Septemba 17, 2018.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (anayeshuhulikia masuala ya Wenye ulemavu), Mhe. Stella Ikupa, akilakiwa na Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba na viongozi wengine, wakati akiwasili kwenye hafla hiyo.
Waziri Mhe. Jenista Mhagama, (katikati), akipokelewa na Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa watu wenye ulemavu Yombo jijini Dar es Salaam, (Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, wakati akiwasili chuoni hapo Septemba 17, 2018.
Wanafunzi wakishangilia
Bw. Mshomba akijadiliana na wasaidizi wake, Mkuu wa Kitengo cha Mawasilianona Uhusiano, Bi. Laura Kunenge, na Afisa Uhusoiano Mwandamizi, Bw. Fulgence Sebera.
Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam, wapili kushoto), huku Naibu Waziri Mhe. Stella Ikupa (kulia), Mkurugenzi Mkuu wa WCF Bw. Masha Mshomba wakishuhudia.
Waziri Mhagama, akimkabidhi mashine hiyo, Kaimu Mkuu wa Chuo cha ufundi kwa wanachuo walemavu Yombo, Bi. Mariam. Kushioto ni Bw. Masha Mshomba.
Picha ya pamoja.
Mmoja wa wanafunzi akionyesha kipaji cha kusakata muziki wa Bongo Flava
Mhe. Jenista Mhagama, akikishajihisha kikundi cha kwaya ya
Mhe, Waziri akimkabidhi mbunge wa Ndanda Mhe. Cecil Mwambe.
Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi mashine mwakilishi kutoka Shule ya Uhuru Mchanganyiko ya Dar es Salaam, Bi.Mwilongo Mtamike.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇