LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2018

UFAFANUZI: SERIKALI YASEMA JUMATATU NI SIKU YA KAZI KAMA KAWAIDA....RAIS ALITANGAZA MAOMBOLEZO, SIO MAPUMZIKO

Serikali kupitia kwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imetoa ufafanuzi kuwa Jumatatu  Septemba 24, 2018  ni siku ya kazi kama kawaida.


Baada ya Rais Magufuli kutangaza siku 4 za maombolezo kufuatia ajali ya MV Nyerere iliyoua watu 166, kumekuwa na mkanganyiko kidogo  kwa baadhi ya watu kudhani Jumatatu itakuwa ni mapumziko.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msigwa amesema Rais Magufuli alitangaza siku 4 za maombolezo  na sio siku za Mapumziko.

Msigwa ameandika;"Napenda kutoa ufafanuzi kuwa Jumatatu tarehe 24 Septemba, 2018 ambayo ni siku ya mwisho ya maombolezo ya Kitaifa, itakuwa ni siku ya kazi kama kawaida. Mhe. Rais Magufuli ametangaza siku 4 za MAOMBOLEZO na sio MAPUMZIKO."

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages