LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 22, 2018

KANGI LUGOLA ASEMA WANAOTUMIA AJALI YA MV NYERERE KAMA MTAJI WA KISIASA WATAKAMATWA

Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola, amewasili katika eneo la tukio kilipozama kivuko cha Mv Nyerere huko Ukara Ukerewe mkoani Mwanza. 

Lugola ametokea mkoani Kigoma ambapo amesitisha ziara yake ya kikazi  na kulazimika kuelekea Jijini mwanza kufuatilia ajali ya MV Nyerere.

Amesema  zoezi la uokoaji na uopoaji litaendelea mpaka hatua ya kivuko kuondolewa majini. 

Pia amesema wote wanaotumia ajali ya Kivuko cha MV Nyerere kama mtaji wa kisiasa watakamatwa na kuchukuliwa hatua kali za kisheria. 

“Hatuko tayari kupitia tukio hili kuchonganisha serikali na wananchi wake, tutakaowabaini tutawakamata”   Amesema Lugola

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages