“Nimeshtushwa na kusikitishwa sana na ajali ya MV Nyerere, nawapa pole wote waliopoteza jamaa zao na nawaombea wote walionusurika kupona haraka, kwa wakati huu nawaomba tutulie wakati juhudi za uokoaji zinaendelea”.... Ni maneno ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Magufuli akitoa pole kwa wahanga wa ajali ya MV. Nyerere mchana wa Leo Septemba 21, 2018.
Salamu hizo zimetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Gerson Msigwa akiwa ameambatanisha na picha ya ajali ya kivuko hicho.
Jana pia Rais Magufuli alitoa salamu za pole kupitia Mkurugenzi Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa wakati wa taarifa ya habari ya saa mbili usiku
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇