Zoezi la ukoaji wa miili ya watu waliopoteza maisha katika Kivuko cha MV Nyerere bado linaendelea ambapo Vikosi Maalum vya uokoaji vya Jeshi la Polisi na Jeshi la Wananchi wa Watanzania (JWTZ) na Jeshi la Zimamoto na uokoaji vinaendesha zoezi hilo.
Idadi ya walipoteza maisha imefikia 100 hadi kufikia saa sita na nusu mchana huu. Kwa mujibu wa DC wa Ukerewe, kivuko hicho kilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 100 na tani 25 za mizigo, lakini kilikuwa na abiria zaidi ya 400.
Kivuko hicho kilizama katika Ziwa Victoria mita 50 kabla ya kutia nanga kisiwa cha Ukara.Kilikuwa kikitokea katika Kisiwa cha Bugolora kuelekea Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇