Ikulu, Dar es
Salaam
Raiswa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Pichani), kuwa Naibu Waziri
wa Wizaraya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Ndumbaro ambaye ni Mbunge wa Songea Mjini Mkoani
Ruvuma anachukua nafasi ya Dkt. Susan Alphonce Kolimba ambayeuteuzi wake
umetenguliwa.
Wakati
huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe
kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Dkt. Mnyepe anachukua nafasi ya Prof. Adolf
Mkenda ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya MaliasilinaUtalii.
Prof. Mkenda amechukua nafasi ya Mej. Jen. Mstaafu Gaudence Milanzi ambaye
amestaafu.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza leo tarehe 26 Septemba,
2018 na tarehe ya kuapishwa kwao itatangazwa baadaye.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇