LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 1, 2018

MAWAZIRI WATATU WAJIUZULU BULGARIA KUFUATIA AJALI Y BARABARANI ILIYOUA WATU 17

Mawaziri wa Usafiri, Ustawi na Mambo ya Ndani nchini Bulgaria, wamejiuzulu nafasi zao ikiwa ni wiki moja tangu kutokea ajali ya barabarani iliyosababisha vifo vya watu 17.
Mawaziri hao waliojiuzulu kufuatia ombi la Waziri Mkuu wa nchi hiyo  Boyko Borisov, ni IvaĂŻlo Moskovski, wa usafiri Nikolay Nankov, wa ustawi wa kieneo na Valentin Radev, wa mambo ya ndani. Kupinduka basi lililokuwa limewabeba watalii wa kigeni karibu na mji wa Sofia, ambao ni mji mkuu wa Bulgaria Jumamozi iliyopita tarehe 25 Agosti na kupelekea watu 17 kufariki dunia na hivyo kuibua radiamali kali na tuhuma za ufisadi wa kifedha wa viongozi wa nchi hiyo, ndio sababu ya mawaziri hao kulazimika kujiuzulu.
Ajali zinazoisakama Bulgaria na kuwalazimisha mawaziri watatu kujiuzulu
Wizara ya Afya nchini humo imetangaza kwamba, watalii 27 wa kigeni pia walijeruhiwa katika ajali hiyo ambapo baadhi yao hali zao ni mbaya sana, ingawa bado uraia wa watalii hao haujatangazwa. Kufuatia tukio hilo, serikali ya Bulgaria ilitangaza siku ya Jumatatu iliyopita ya tarehe 27 Agosti kuwa siku ya maombolezo ya kitaifa. Mwaka jana kituo cha takwimu cha Umoja wa Ulaya kilielezea ongezeko kubwa la ajali za barabarani nchini Bulgaria na hivyo kuifanya nchi hiyo kushika nafasi ya pili baada ya Romania, kwa kuwa na kiwango cha juu cha ajali za barabarani ikilinganishwa na nchi nyingine za umoja huo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages