LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 15, 2018

MASHAMBULIO YA ANGA YA SAUDIA DHIDI YA GHALA LA WFP HUKO YEMEN

Ndege za kivita za muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia zimelishambulia ghala la kuhifadhia chakula la Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika mji wa al Hudaydah.
Muhammad Ali al Houthi Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi ya Yemen amesema kuwa kitendo cha kushambulia ghala la shirika la WFP huko al Hudaydah kinaonyesha kuwa maghala, stoo za kuhifadhia chakula na makazi ya raia yamekuwa maeneo halali ya kulengwa na mashambulizi ya anga ya Saudia na washirika wake nchini Yemen. 
Muhammad Ali al Houthi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Mapinduzi Yemen 
 
Shirika la WFP ni tawi la kusambaza misaada ya chakula la Umoja wa Mataifa. Mwaka 1961 Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO) na Baraza Kuu la umoja huo yalipasisha azimio la kuasisi shirika la WFP na mwaka 1963 Shirika la Mpango wa Chakula Duniani likaundwa. Usambazaji misaada ya chakula ni moja ya nyenzo zinazoimarisha usalama wa chakula. Usalama wa chakula una maana kuwa watu wote na siku zote wana haki ya kupata bidhaa za chakula wanazohitajia ili kuweza kuishi katika mazingira salama, katika hali ya kawaida na ya mgogoro.
Hatua ya Saudi Arabia ya kuvishambulia vituo na taasisi za kimataifa likiwemo Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) inaonyesha kuwa nchi hiyo haina mipaka katika kufanya jinai dhidi ya watu wa Yemen. Upuuzaji wa Umoja wa Mataifa hususan Baraza la Usalama la umoja huo pia umeipa Saudi Arabia kiburi cha kukanyaga sheria na maazimio ya kimataifa na kuamua kuzidisha jinai zake huko Yemen. Wakati huo huo hatua ya jamii ya kimataifa ya kufumbia macho vitendo vya kigaidi vya wanajeshi vamizi wa Saudi Arabia imewatia kiburi zaidi wavamizi hao cha kutenda uhalifu na jinai zaidi dhidi ya raia wa Yemen.   
Hali ya wasiwasi imetanda kuhusu kushadidi maafa yanayosababishwa na muungano huo huko Yemen ikiwa imepita miezi kadhaa sasa tangu muungano huo vamizi  unaoongozwa na Saudi Arabia uizingire kwa pande zote nchi hiyo ya Kiarabu. Mzingiro huo mkubwa dhidi ya Yemen umeifanya nchi hiyo ikabiliwe na uhaba mkubwa wa chakula, dawa na kukumbwa na milipuko ya magonjwa ya aina mbalimbali na hivyo kusababisha maafa ya kibinadamu. Wakati huo huo hatua ya Saudia ya kufunga vivuko huko Yemen na vilevile kuyashambulia maghala ya kuhifadhia chakula ni ishara ya wazi wa kuwaadhibu kwa umati raia wa nchi hiyo. Kuhusiana na suala hilo azimio lililopasishwa na Umoja wa Mataifa linalopiga marufuku mauaji ya kizazi linaitaja hatua yoyote katika uwanja huo kuwa ni jinai na inasisitiza kwamba wahusika wa jinai hizo wanapaswa kuadhibiwa.  
Milipuko ya magonjwa inayowasibu wananchi wa Yemen
Katika ripoti yake ya hivi karibuni kundi la kimataifa na kieneo la wataalamu wanaojitegemea linalowajumuisha Charles Galoway kutoka Uingereza, Camel Jundubi kutoka Tunisia na Melisa Park wa Australia ambalo liliundwa tarehe 4 Disemba mwaka jana kufuatia ombi la Kamati Kuu ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa limeashiria ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kushambuliwa vituo na taasisi za kimataifa katika mashambulizi ya anga ya kuogofya eti ya muungano wa Saudi Arabia Yemen. 
Tunapotupia jicho mgogoro wa Yemen tunaona kuwa Saudi Arabia imefanya mauaji ya umati ya aina zote ikiwa ni pamoja na kufanya mashambulizi ya anga dhidi ya makazi ya raia na kuiwekea nchi hiyo mzingiro mkubwa wa pande zote; na ni dhahir shahir kuwa mgogoro huo umewatumbukiza wananchi wa Yemen katika maafa makubwa ya binadamu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages