Baada ya hivi karibuni Waziri mkuu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa kutembelea na kukagua ujenzi wa barabara za juu (flyover), eneo la Tazara Dar es salam na kusema umekamilika kwa asilimia 98, hatimaye leo barabara hizo zimeanza kutumika.
Msemaji mkuu wa serikali Dkt. Abbas Hassan, amethibitisha kuwa kuanzia leo serikali imeruhusu rasmi matumizi ya barabara hizo hadi pale uzinduzi utakapofanyika mwezi ujao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alitembelea barabara hizo za juu tarehe 29/8/2018, katika makutano ya Barabara ya Mandela na Nyerere (Tazara) na kusema mradi huo umekamilika kwa asilimia 98.
Katika ziara yake hiyo Majaliwa aliweka wazi kuwa wakati wowote kuanzia Oktoba, 2018, Rais John Magufuli atazindua barabara hiyo ambayo imepewa jina la Mhandisi Patrick Mfugale.
Serikali ya Tanzania ilisaini mkataba wa ujenzi wa barabara hizo na Kampuni ya Sumitomo Mitsui Construction ya Japan mwaka 2015 na kueleza kuwa mradi huo utagharimu zaidi ya Sh87 bilioni.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇