LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 6, 2018

KESI YA KWANZA YA EBOLA YARIPOTIWA BUTEMBA, MASHARIKI MWA JAMHURI YA KIDEMOKRASIA YA CONGO

Kesi ya kwanza ya maambukizi ya ugonjwa hatarai wa Ebola imeripotiwa katika mji wa Butembo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Kuripotiwa kwa kesi ya kwanza ya maambukizi ya Ebola huko Butembo kumezua wasiwasi mkubwa hasa kwa kutilia maanani kwamba, mji huo una wakazi wanaokaribia milioni moja na ambao ni kiungo cha biashara kati ya nchi hiyo na nchi jirani ya Uganda.
Tangazo la kesi ya kwanza ya maambukizi ya maradhi ya Ebola katika mji wa Butembo limetolewa na Dakta Oly Ilunga Kalenga, Waziri wa Afya wa nchi hiyo ambaye ameeleza kuwa, tayari wizara yake imechukua hatua za kukabiliana na mlipuko huo mpya wa Ebola.
Mji wa Butembo unahesabiwa kuwa muhimu mno hasa kutokana na kuwa bidhaa nyingi zinazoingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kutokea Afrika Mashariki zinapitia katika mji huo.
Daktari akimpatia chanzo mmoja wa raia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
Sylvain Kanyamanda, Meya wa Butembo amewataka wakazi wa mji huo kuchunga na kufuata miiko yote ya kiafya ya kujikinga na maradhi hayo.
Mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola uliripotiwa DRC Agosti 1 wiki moja tu baada ya WHO kutangaza kuwa mlipuko wa awali wa ugonjwa huo umedhibitiwa. 
Tangu mwaka 2014 hadi hivi sasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeshakumbwa mara kadhaa na wimbi la ugonjwa hatari wa Ebola.
Katika kipindi cha baina ya mwaka 2013 hadi 2016, virusi hatari vya Ebola vilichukua roho za karibu watu 11 elfu katika maeneo tofauti duniani.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages