Mkuu wa Wilaya ya Newala Aziza Mangosongo (mwenye pama), akishiriki utoaji chanjo ya ugonjwa wa kideri kwa kuku alipozindua uchanjaji huo katika kijiji cha Chihangu Wilayni Newala.
NEWALA, MTWARA
Mkuu wa Wilaya ya Newala mkoani Mtwara Aziza Mangosongo amelipongeza shirika la Agakhan Foundation kwa kuwajengea uwezo wakulima katika Wilaya hiyo.
Pamoja na pongezi hizo Mkuu huyo wa Wilya amesema Programu zitasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua hali ya kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja, vikundi na jamii ya wananchi wa Newala kwa jumla.
Mkuu huyo wa wilaya alisema hayo mapema wiki hii, akiwa katika ziara ya mafunzo, Agosti 27, 2018, ambapo aliongozana na timu ya Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Newala ili kujionea miradi ya vikundi vya wananchi katika Halmashauri hivyo.
Katika ziara hiyo, Mkuu huyo wa wilaya aliongozana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Rashidi Ndembo , Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mussa Chimae, Madiwani wawili wa Halmashauri ya Wilaya pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya.
Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na ujumbe wake walitembelea Shirika lisilo la Kiserikali la Aghakani Foundation (ARF) linaloendesha Program ya Ajira na Ujuzi (Employment and Skills) inayolenga kuwawezesha Kaya zipatazo 5000 za wakulima wadogowadogo kujiongezea kipato, kujipatia chakula na kuongeza uzalishaji mali na kuongeza thamani ya mazao yao kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Programu hiyo inayo miradi ijulikanayo kama Kilimo ni Biashara unaotekelezwa katika Wilaya ya Newala kuanzia April 2016 hadi Machi 2018, chini ya ufadhili wa shirika la Kijerumani lisilo la Kiserikali la GTZ.
Mkuu huyo wa Wilaya ya Newala alitembelea Vijiji vya Chihanga, Idamnole, Tengulengu na Kitangari, mbapo akiwa katika Kijiji cha Chihangu yeye na msafara wake walikutana na vikundi vya wakulima wanaofadhiliwa na Aghakhan Foundation katika miradi ya kuongeza kipato kwa kufuga kuku wa kienyeji kisasa, akashiriki kuzindua chanjo ya ugojwa wa kideri wa kuku unaoelezwa na wataalamu kuwa ndiyo ugonjwa hatari wa kuambukiza unaorudisha nyuma usalishaji wa kuku katika Wilaya ya Newala.
Akiwa katika Kijiji cha Idamnole Kata ya Chihangu alikagua shughuli ya ukamuaji wa mafuta ya Alizeti unaofanywa na wakulima katika vikundi vilivyo chini ya mradi wa kilimo Biashara unaofadhiliwa pia na Aghakan Foundation, ambko aliona ujenzi wa nyumba bora ya mkulima unaotokana na uzalishaji na bei nzuri ya mauzo ya zao la korosho katika Mkoa wa Mtwara, hususani Wilaya ya Newala.
Tangu Serikali ya awamu ya tano chini ya Eais Dk. Jonh Magufuli iingie madarakani bei ya zao la korosho imepanda na kuimarika hivyo kuwezesha wananchi kadhaa wa Wilaya ya Newala kujenga nyumba nzuri na za kisasa, Vijijini.
Baadae msafara ulielekea katika Kata ya Kitangari Kijiji cha Kitangari Tarafa ya Kitangari ambapo ulifika kwa Wafugaji wawili wa kuku wanaofadhiliwa na Agakhan Foundation, wakulima hao wameweza kuongeza uzalishaji wa kuku kiasi cha kufuga hadi kuku 800 wa chotara ambao kwa wastani mmoja huuzwa Sh.20,000 hadi Sh. 25,000 baada ya kuhudumiwa kwa miezi minne tu.
Agosti 28, 2018, Mkuu huyo wa Wilaya Newala alitembelea miradi ya kilimo cha Mbogamboga katika bonde la Chiunjila katika Kijiji cha Chihanga Kata ya Mkunya na kisha kwenda Kijiji cha Mapili ambako alikutana na mkulima wa nyanya na mfugaji wa kuku wa kienyeji ambaye anafuga kisasa baada ya kupata mafunzo kutoka shirika lisilo la Kiserikali la Agakhan Foundation.
Mkuu wa Wilaya alihitimisha ziara yake katika Kijiji cha Nanguruwe.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Aziza Mangosongo akiwa na ujumbe aliokuwa nao katika ziara hiyo.
Your Ad Spot
Aug 30, 2018
Home
Unlabelled
ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA NEWALA KATIKA MIRADI YA KILIMO BIASHARA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LA AGAKHAN FOUNDATION
ZIARA YA MKUU WA WILAYA YA NEWALA KATIKA MIRADI YA KILIMO BIASHARA INAYOFADHILIWA NA SHIRIKA LA AGAKHAN FOUNDATION
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇