LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 30, 2018

DC ANAMRINGI MACHA AOMBA MADIWANI MSALALA KUTUNGA SHERIA ZITAKAZOWABANA WAZAZI WATOE MAHITAJI YA SHULE KWA WATOTO WAO

Mkuu wa wilaya  ya Kahama mkoani Shinyanga Anamring Macha (pichani) amewaomba madiwani wa Halmashauri ya Msalala kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wazazi ili waweze kuwahudumia watoto wao mahitaji ya shule kikamilifu.

Macha ametoa wito huo wakati akiwahutubia madiwani wa hakmashauri hiyo katika baraza LA madiwani lililoketi agosti 30 katika ukumbi wa halmashauri hiyo.

Mkuu huyo  amesema ni aibu kwa wilaya  ya kahama kuwakuta watoto wakiwa wanaenda shule bila mshitaji maalulu kama vile viatu,winifomu,kalamu na madafutari huku wazazi wao wakiwa wanamiliki mfungo mingi ambayo haina msaada kwa watoto.

Aidha ameongeza kuwa iwapo madiwani watatunga sheria itakayowaruhusu viongozi kuuza mfugo ya wazazi na kuwanunulia watoto mahitaji ya shule kwa kila mtoto ambaye watamkuta hana mahitaji mhimu hiyo itasaidia wazazi kuwahudumia watoto wao na kuinua kiwango cha elimu.

Pia Hakimu mkazi wa mahakama ya mwanzo ya busangi mhe. Julias  Sisa  amemuhapisha diwani mpya wa kata ya bugarama mheshimiwa Josephat  Izengo aliyeubuka na ushindi katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika agosti 12 mwaka huu kufuatia diwani hiyo kukihama chama chake cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) na kujiunga na chama cha mapinduzi (CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages