Na Ahmed Mahmoud Arusha
Kampuni za Bima nchini zimesisitizwa kuepuka kutoa huduma kimazoea badala yake kutoa huduma ya bima kwa makundi yaliyo sahaulika yakiwemo ya wakulima kwa kutoa mikopo ili kufikia uchumi wa kati .
Kauli hiyo imetolewa jana Agost 27, jijini Arusha na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk, Ashatu Kijaji wakati alipofungua mkutano wa 41 wa Umoja wa Kikanda wa Makampuni ya Bima ya Nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika (OESAI) unaoshirikisha nchi 39.
Dk, Kijaji alisema asilimia 75 ya Watanzania ni wakulima ambao bado hawana elimu juu ya bima ikiwemo kupata mikopo ya bei nafuu kwaajili ya kutatua changamoto za kilimo na kufikia katika uchumi wa kati.
Alitoa rai kwa makampuni ya bima nchini kuangalia kundi hilo la wakulima ili nao waweze kunufaika na bidhaa wanazozalisha kwakuwa kundi hilo ni kubwa na ni fursa kwa makampuni ya bima nchini kuongeza idadi ya watumiaji wa bima.
Alisisitiza kuwa watanzania wanatumia bima ni chini ya asilimia moja idadi ambayo hairidhishi kabisa kwakuwa watanzania wapo zaidi ya milioni 45 kwa mujibu wa Takwimu za Taifa.
Naye Kamishna wa Bima wa Mamlaka ya Usimamizi wa Shughuli za Bima Nchini (TIRA) Dk, Baghayo Saqware alisema mkutano huo ni wa 41 kufanyika hapa nchini ambapo mkutano wa mwisho ulifanyika mwaka 1995 na kusisitiza kuwa mkutano huo unatoa fursa kwa kampuni za bima zilizopo hapa nchini kujifunza jinsi kampuni za nje the bima zinavyofanya kazi kwa ufanisi.
Pia kampuni hizo zitapata fursa ya kujifunza uboreshaji wa huduma kwa kutumia mfumo wa Tehama unaoleta mageuzi katika utoaji wa huduma bora zako bima, rasilimali watu, kuongeza wigo wa kutafuta watu mbalimbali kwaajili ya kulipia bima ya maisha.
Naye Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya mkutano huo,Khamis Suleiman alisema lengo la mkutano huo ni kuhakikisha ifikapo mwaka 2020 asilimia 50 ya watanzania wawe na aina yoyote ya bima kwani kwa sasa Tanzania ipo kwenye nafasi ya pili kwa nchi za Afrika Mashariki kwa kutoa huduma za bima.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇