Mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga, Gwakisa Kasongwa akizungumza katika Warsha ya ufunguzi wa mradi wa kuongeza utumiaji wa uzazi wa mpango mkoani Tanga ulipo chini ya usimamizi wa wadau Jhpiego ambao umepangwa kutekelezwa katika Halmashauri tatu mkoani humo katika Halmashauri za Mji na ya Vijijini za Korogwe na Halmashauri ya Jiji la Tanga Mji. Kulia ni Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.
Lengo la mradi ni huo kuboresha afya na mama na mtoto na kuhakikisha vifo vya watoto na kinamama inapungua 'better reproductive health care'.
Korogwe kupitia mkuu wa wilaya yake Gwakisa (Kissa) Kasongwa walimwahidi Waziri wa Afya Ummy Mwalimu, kwamba watahakikisha miradi itakayoanzishwa Korogwe itakua endelevu 'Sustainablity' na Usimamizi dhahiri na Madhubuti.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Gwakisa na viongozi wengine baada ya semina hiyo |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇