LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Aug 30, 2018

RAIS MSTAAFU ALHAJI ALI HASSAN MWINYI AMTEMBELEA WAZIRI KIGWANGALLA (MOI)

 Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Respicious Boniface akimpokea Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi mara alipomtembelea Waziri wa Maliasili Dkt. Kigwangalla ambaye anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Mifupa 
(MOI).

RAIS Mstaafu wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi leo Agosti 29,2018 amemtembea na kumuombea dua maalum Dkt Hamisi Kigwangalla ambaye anapata matibabu katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI akiuguza majeraha ya mkono aliyopata katika ajali iliyotokea Agosti 4, mwaka huu Mkoani Manyara.

Mzee Mwinyi aliambatana na Mkewe Bi. Siti Mwinyi ambapo wamemjulia hali pamoja na kufanya dua hiyo ili aweze kupona haraka kurejea kwenye majukumu yake ya kitaifa.

“Nimefika leo kukujulia hali na upokee dua hii upone haraka. Sisi tunaendelea kukuombea muda wote kwa muumba” alieleza Mzee Mwinyi.

Kwa upande wake Dkt. Hamis Kigwangalla amemshukuru Mzee Mwinyi na Mama Mwinyi kufika kumjulia hali ambapo awali alimuelezea kuwa anaendelea vizuri na muda wowote ataruhusiwa.

“Nashukuru kufika kwenu na sasa naendelea na mzoezi vizuri huku kubwa nikisubiria ruhusa ya Madaktari wanaoendelea kunipatia matibabu” alieleza Dkt. Kigwangalla.

Katika hatua nyingine kwa sasa Dkt. Kigwangalla afya yake imeendelea kuimarika zaidi ambapo jana jioni ya Agosti 28, ameweza kutembea umbali wa zaidi ya Kilometa Nane ambapo hii ni hatua nzuri kwani kila siku amekuwa akiongeza umbali wa kutembea kwa lengo la kufanya mazoezi ya viungo vyake.


Dkt Kigwangalla alihamishiwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI tarehe 12/08/2018 baada ya kupata matibabu ya awali katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwa sasa bado anaendelea na tiba kuuguza mkono wake wa kushoto.


 Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Kaimu Meneja wa jengo, Elizabeth Mbaga wakati alipomtembelea Waziri wa Maliasili Dkt. Kigwangalla katika Taasisi ya Mifupa 
(MOI), wa tatu kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Respicious Boniface na anaye fatia ni Dkt. Kennedy Nchimbi 
  Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Kaimu Meneja wodi za kulipia, Maagreth kumpuni 
  Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Waziri wa Maliasili Dkt, Hamisi Kigwangalla mara alipomtembelea katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambapo anapatiwa matibabu 
 Mama Sitt Mwenyi akimsalimia Waziri wa Maliasili Dkt, Hamisi Kigwangalla mara alipomtembelea katika Taasisi ya Mifupa (MOI) ambapo anapatiwa matibabu
 Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi 
(katikati) akiongoza dua maalumu kumuombea Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt, Hamisi Kigwangalla mara alipomtembelea na kumjulia hali katika Taasisi ya Mifupa 
(MOI), Watatu kulia ni mama Sitt Mwenyi na Viongozi wa Taasisi hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Respicious Boniface (wa pili kushoto)

  

Rais Mstaafu wa Awamu ya pili Mzee Ali Hassan Mwinyi (katikati) akizungumza jambo alipomtembelea na kumjulia hali Waziri Kigwangalla katika Taasisi ya Mifupa MOI anapopatiwa matibabu.kushoto ni mama Siti Mwinyi. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages