Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana, akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (wa pili kulia), na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka (kulia), kuhusu hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kitengo cha mizani iliyopo eneo la Makambako mkoani humo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Njombe Mhandisi Yusuph Mazana (wa tatu kushoto), wakati akikagua nguzo ya daraja la mto Halali katika barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 wilaya ya Wanging'ombe, mkoani humo. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, akisikiliza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, (wa kwanza) na Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka, wakitoka kukagua kingo za daraja la mto Halali lililopo katika barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 wilaya ya Wanging'ombe, mkoani humo.
Kaimu Mhandisi Mkazi kutoka kampuni ya LEA JV South Asia, Manish Kumar (kushoto), akimuonesha ramani Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (katikati), wakati akikagua ujenzi wa barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole-Sendeka akifuatilia.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe, akisalimiana na mkazi wa kijiji cha Ilembula wilaya ya Wanging'ombe Bi. Hadija Samuli, wakati alipokuwa akikagua barabara ya Nyigo-Igawa yenye urefu wa KM 64.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe.
Muonekano wa sehemu ya barabara ya Nyigo-Igawa KM 64.6 inayojengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Njombe. Mradi wa ujenzi huo utakamilika mwezi Disemba mwaka huu na utagharimu kiasi cha zaidi ya Shilingi bilioni 103.(PICHA NA WUUM)
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇